PERMISSIONS

WHO: Nchi tajiri zinadhoofisha mpango wa kugawa chanjo ya corona kwa usawa

1 week ago 11

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO amezishutumu 'baadhi ya nchi tajiri' kuwa zinadhoofisha mpango wa COVAX na ugawaji wa chanjo ya corona kwa usawa.

Tedros Adhanom ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya kwa njia ya intaneti na Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani na akabainisha kuwa, hivi sasa baadhi ya nchi tajiri zinaendelea kuwasiliana kwa karibu na watengenezaji wa chanjo ya corona ili kuhakikisha zinapata dozi nyingi zaidi za chanjo hiyo.

Adhanom ameongeza kuwa, jambo hili linaathiri makubaliano yaliyofikiwa na mpango wa COVAX na kwa sababu hiyo linapelekea kupungua idadi ya dozi zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mpango huo unaosimamia ugawaji wa chanjo ya corona kwa usawa.

Mpango wa COVAX umeanzishwa ili kuhakikisha nchi tajiri duniani hazihodhi dozi zote za chanjo ya corona ambazo kwa sasa zinapatikana kwa kiwango maalum na kutoweza kukidhi mahitaji ya ulimwengu mzima. Mpango huo unasimamia pia utaratibu wa kupatia fedha na kuandaa mazingira kwa nchi 92 zenye kipato cha chini na cha kati duniani ya kuweza kupata chanjo hiyo ya kujikinga na maradhi ya Covid-19.../

Read Entire Article