PERMISSIONS

Wanne watiwa mbaroni Tanzania kwa kueneza habari za vifo vya corona

1 week ago 8

Watu wanne wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Pwani nchini Tanzania kwa tuhuma za kueneza uvumi wa vifo vya watu waliokufa kwa corona, kupitia mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi Pwani, Wankyo Nyigesa, amethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, watu hao wamekamatwa kutokana na kueneza hofu katika jamii na wengine wanaendelea kutafutwa na jeshi hilo kwa tuhuma hizo hizo.

Nyigesa amesema, watu hao wanakabiliwa pia na tuhuma za kupendekeza majina ya viongozi wa serikali ambao walitamani wafe haraka kwa corona.

Amesema: “Licha ya kueneza uvumi wa vifo vya watu wakidai wamekufa kwa corona, pia wanatia hofu mitandaoni kwa kudai Watanzania walio wengi watakufa kwa sababu serikali haichukui tahadhari dhidi ya wananchi wake."

Amewataja waliokamatwa kuwa ni Frank Nyange (47), Moses Goodluck (34), Mohammed Abdallah Lutambi (45) na Bumija Moses (55) ambao ni viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Juzi Jumamosi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa (WHO) Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus alituma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Tanzania kwa msiba wa Katibu Mkuu kiongozi wa serikali uliotokea mapema juma hili na wakati huo huo akaitaka serikali Tanzania itoe takwimu ya corona kama zinavyofanya nchi nyingine. 

Huku hayo yakiripotiwa, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amepiga marufuku kufanyika shughuli za maziko kwa kutumia magari ya matangazo ya vifo mitaani, ambayo yamekuwa yakianzia mochwari mpaka nyumbani kwa marehemu kitu ambacho kimelalamikiwa kuleta usumbufu kwa wakazi wa mkoa huo.

Chalamila amesema: “Wananchi wa Mbeya wamekuwa wakipitisha magari ya matangazo mitaani wakati wa misiba huku wakitaja wasifu wa Marehemu, picha ya Marehemu ikiwa mbele ya gari na msafara ukifuata, hii imetajwa kuwasumbua wengine, ninaagiza kuanzia Februari 24, 2021, tabia hiyo ikome.” 

Read Entire Article