PERMISSIONS

Wanasiasa wa upinzani Somalia waakhirisha maandamano dhidi ya serikali

1 month ago 34

Wanasiasa wa upinzani nchini Somalia wameakhirisha maandamano yao waliyokuwa wamepanga kufanya leo Ijumaa baada ya Waziri Mkuu kuingilia kati.

Wanasiasa wa upinzani nchini Somalia wameakhirisha maandamano hayo waliyopanga kufanya leo Ijumaa mjini Mogadishu baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohamed Hussein Roble kukubali baadhi ya matakwa yao.

Maandamano hayo ambayo yalipangwa na wapinzani wa serikali ya Somalia licha ya serikali kuyapiga marufuku kwa lengo la kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa wa Covid-19, hatimaye yameakhirishwa baada ya Waziri Mkuu Hussein Roble kueleza rasmi kwamba amesikitishwa na ghasia zilizojitokeza Ijumaa wiki iliyopita katika maandamano kama hayo ya upinzani. 

Viongozi wa upinzani nchini Somalia wamekubaliana kuakhirisha maandamano hayo siku moja baada ya serikali kuu ya Mogadishu kusema kuwa, itachunguza shambulio lililotekelezwa katika hoteli moja ambako viongozi mbalimbali walikuwa wiki iliyopita.  

Juzi Baraza la Wagomgea Urais wa Kambi ya Upinzani nchini Somalia lilitahadharisha kuwa, litaendelea na maandamano ya amani ili kueleza waziwazi upinzani wao kwa serikali ya Rais Mohamed Farmajo, kupinga suala la kuendelea kuwepo madarakani Rais huyo kinyume cha sheria na kuchelewesha chaguzi za Rais na Bunge.

Rais Mohamed Farmajo wa Somalia 

Muhula wa rais wa sasa Mohamed Abdullahi Mohamed, maarufu kama Farmaajo, ulimalizika Februari 8 lakini kutokana na mgogoro wa kisiasa, Bunge linalomchagua rais bado halijachaguliwa. 

Serikali ya Somalia ilipiga marufuku maandamano ya wapinzani katika mji mkuu Mogadishu kutokana na ongezeko la maambukizi ya corona na tishio la usalama. 

Read Entire Article