PERMISSIONS

Wanafunzi waliotekwa Nigeria waachiliwa

1 week ago 13

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, wanafunzi hao kutoka shule ya upili ya Government Day wameachiliwa kwa msaada wa baadhi ya watekaji nyara waliojisalimisha. Tukio hilo lilifanyika Septemba mosi baada ya watu wenye silaha kuvamia shule hiyo,ikiwa ni moja ya matukio ya karibuni ya utekaji nyara, yaliyopelekea serikali kufunga shule zote za msingi na sekondari kwenye jimbo la Zamfara.

Kulingana na shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF,Nigeria imeshuhudia taktiban visa 10 vya aina hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo takriban wanafunzi 1,436 wametekwa. Zaidi ya wanafunzi 200 wanaendelea kushikiliwa huku 16 wakisemekana kufa wakati wa mashambulizi. Matukio mengi yanasemekana kufanyika kwenye majimbo 9 mengi yakiwa kaskazini mwa Nigeria.

Read Entire Article