PERMISSIONS

Wafungwa zaidi ya 200 watoroka jela nchini Nigeria

1 week ago 13

Wafungwa zaidi ya 200 wanaripotiwa kutoroka katika jela moja nchini Nigeria huko magharibi mwa Afrika.

Maafisa katika jimbo la Nigeria la Kogi  wanasema kuwa, wafungwa v240 wametoroka baada ya watu wenye silaha kuvamia gereza katika eneo la Kabba-Bunu. Mamlaka ya huduma za magereza nchini Nigeria imesema katika taarifa yake baada ya tukio hilo kwamba,  washambuliaji walikuwa wamejihami kwa silaha.

Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa maafisa wawili wa usalama wameuawa wakati wa tukio hilo.

Taarifa zinasema kuwa, wakati wavamizi walipofika, walikabiliana na walinzi wa gereza, na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani ya gereza baada ya kuwazidi nguvu maafisa wa usalama wa ngereza hilo.

Mamlaka ya huduma za magereza nchini Nigeria imesema kuwa, kulikuwa na jumla ya wafungwa 294 katika gereza hilo wakati shambulio lilipotokea, na kwamba, 240 kati yao walikuwa wakisubiri kesi zao, na 70 walikuwa tayari wameshhukumiwa.

Rais Muhamadu Buhari wa Nigeria

Kamishna mkuu wa magereza Halliru Nababa ametoa agizo la kusakwa na kukamwatwa wafungwa waliotoroka.

Wakati huo huo, makumi kadhaa ya watoto waliokuwa wametekwa nyara na watu wenye silaha kaskazini mwa Nigeria karibu wiki mbili zilizopita wameokolewa.

Matukio ya utekaji nyara hasa dhidi ya wanafunzi yamekithiri mno katikka miezi ya hivi karibuni nchini Nigeria ambapo watekaji nyara hudai pesa kama kikomboleo cha kuwaachia huru matekak wao.

Read Entire Article