PERMISSIONS

Wafugaji 100 wauawa katika mapigano ya kugombania ardhi Ethiopia

1 week ago 18

Mapigano baina ya wafugaji wa jamii hasimu zinazopakana katika eneo la Afar na Somali kaskazini mashariki mwa Ethiopia yamepelekea watu zaidi ya 100 kuuawa.

Ahmed Humed, Naibu Kamishna wa Polisi katika eneo la Afar ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, takriban raia 100 aghalabu yao wakiwa ni wafugaji, wameuawa katika mapigano hayo yaliyoibuka Ijumaa katika mpaka wa eneo hilo la Somali.

Ameongeza kuwa, mpaka jana Jumanne, makabiliano baina ya pande mbili hasimu yalikuwa yanashuhudiwa katika eneo hilo la mpakani. Afisa huyo wa polisi amevilaumu vikosi vya usalama kutoka eneo jirani la Somali kwa mapigano hayo.

Naye msemaji wa eneo la Somali, Ali Bedel amesema watu 25 waliuawa katika ghasia za Ijumaa katika eneo hilo, huku akiituhumu jamii ya Somali kuwa ndio walioanzisha mapigano hayo. Haijabainika iwapo 25 hao ni miongoni mwa watu 100 waliouawa kufikia sasa katika mapigano hayo yanayoonekana kuwa ya kikabila au la.

Mapigano ya kikabila yanaripotiwa huku hali ikiwa ingali tete katika eneo la Tigray

Haya yanajiri wiki moja baada ya watu waliokuwa na bunduki kuwauwa raia wasiopungua 30 katika shambulio lililolenga kijiji kimoja katika mkoa wa Oromia nchini Ethiopia. Shambulizi hilo linatambuliwa kuwa ni katika mfululizo wa ghasia za kikabila za hivi karibuni za wapinzani wa serikali ya shirikisho.

Mapigano na ghasia zimeshika kasi nchini Ethiopia kufuatia kuongezeka mapigano ya kikabila hususan katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Mapigano hayo ya kikabila nchini Ethiopia, mbali na kusababisha mamia ya raia kuuawa, lakini yamepelekea pia mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.

Read Entire Article