PERMISSIONS

Virusi vya corona: Jinsi Kremlin inavyomlinda Rais Putin dhidi ya maambukizi

1 week ago 10

Dakika 1 iliyopita

Presidente Putin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais wa Urusi Vladmir Putin

Kuanzia mwanzo wa janga la corona, mamlaka nchini Urusi zimefanya kila linalowezekana kumlinda Rais Vladimir Putin kutokana na maambukizo ya ugonjwa huo. Lakini unaandaaje karantini ya mtindo wa Kremlin na kwa gharama gani?

Katika mwaka uliopita, mamia ya watu walilazimika kujitenga nchini Urusi, kabla ya kumkaribia Vladimir Putin.

Wengine walilazimika kujitenga hata ikiwa hawakutangamana moja kwa moja na rais, lakini kama tahadhari kwa sababu walikuwa wakitangamana na watu wengine ambao walikuwa wanapanga kukutana naye.

Mnamo Machi 25, 2020, Rais Putin alihutubia taifa na kutangaza kwamba Aprili 1 itaashiria mwanzo wa “wiki isiyo ya kufanya kazi,” wakati coronavirus ilipoenea haraka nchini Urusi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

El Kremlin ha hecho grandes esfuerzos económicos y logísticos para mantener a Putin a salvo de la enfermedad.

Baadaye, mnamo Aprili, masharti ya kutotoka nje yalianzishwa na kufungwa kwa maduka yasiyo ya mahitaji muhimu na kupigwa marufuku kwa mikusanyiko ya watu wengi, huku watu wakianza kufanyia kazi nyumbani.

Wakati huo huo, wanachama 60 ambao ni wafanyikazi maalum wa ndege ya shirika la Rossiya, wanaomhudumia Rais Putin na maafisa wengine wakuu wa serikali ya Urusi, walitengwa kwa mara ya kwanza mnamo Machi 26, 2020 katika hoteli karibu na mji wa Moscow.

Tangu wakati huo, mamia ya marubani, madaktari, madereva na wafanyikazi wengine wanaohudumu karibu na rais na pia wageni wa rais, wamekuwa katika karantini wakijitenga katika hoteli kadhaa nchini Urusi kumlinda Rais Putin kutokana na maambukizi.

Hivi karibuni, iliripotiwa kuwa rais alipokea chanjo iliyotengenezwa nchini Urusi, ingawa haijabainishwa ni ipi, lakini mikataba na hoteli kadhaa za “karantini” inaonekana kuwa itatumika hadi mwaka ujao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Antes de que Putin asista a actos públicos se toman numerosas medidas para minimizar el riesgo de que se contagie.

BBC Idhaa ya Irusi inakadiria kwamba Kurugenzi ya Rais wa Shirikisho la Urusi, kitengo kinachohusika na utendaji mzuri wa timu ya rais, kilipokea karibu Dola za Kimarekani milioni 84 kutoka bajeti ya serikali kwa shughuli za kupambana na janga hilo.

BBC imegundua kwamba angalau, hoteli 12 zimetumika kwa karantini kwa wahudumu wa Kremlin.

Sehemu hizi za malazi ziko Moscow na mkoa wake wa karibu, Eneo la Crimea ambalo Urusi ilichukua kimabavu, na pia katika eneo lisilo mbali na mji wa kusini wa Sochi, Mji wa mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi mwaka wa 2014 na moja ya maeneo yanayopendwa sana na Putin.

Mahali pote ambapo wageni na wafanyikazi wanaomhudumia walitumia ni sehemu zilizoandikwa kuwa makao ya rais . Baadhi ya maeneo hayo yamekodishwa hadi Machi 2022

Wafanyikazi wa ndege wa Rossiya wanaonekana kuwa ndio wageni wakuu wa hoteli hizi.

Wafanyikazi hao wanawahudumia maafisa wa ngazi ya juu, pamoja na Rais Vladimir Putin mwenyewe, Waziri Mkuu Mikhail Mishustin na mawaziri wengine wanane wa baraza la mawaziri.

Chanzo cha picha, Kremlin.ru

Maelezo ya picha,

Detrás de las apariciones de Putin en público hay toda una operación para asegurar que no corre riesgo de infectarse con el coronavirus.

Idhaa ya BBC Urusi iligundua kuwa Rais Putin alifnya kazi kwa muda mrefu mwaka jana akiwa katika makazi yake ya Sochi.

Duru zinazofahamu hali ya karantini hiyo zilisema kwamba marubani kadhaa na wafanyikazi wengine wa anga waliwekwa karantini karibu na Sochi kutoa usafiri kwa rais, na vile vile kwa waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje na wengine wengi.

Miongoni mwa wale waliotengwa walikuwa marubani wa ndege na helikopta.

Read Entire Article