PERMISSIONS

UNHCR yahimiza kuokolewa haraka wakimbizi Waislamu Warohingya waliokwama majini

1 week ago 3

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limetoa wito wa kutafutwa na kuokolewa haraka kundi la wakimbizi Waislamu Warohingya ambao wamekwama katika meli kwenye eneo la maji la Andaman kwa zaidi ya wiki moja.

Indrika Ratwatte, Mkurugenzi wa UNHCR Ofisi ya Kanda ya Asia na Pasifiki, amesema idadi kamili na eneo la waathirika bado halijajulikana, na inaripotiwa kuwa watu wengi wanaweza kuwa wamekufa.

Ratwatte amesema, "kwa sababu ya ukosefu wa habari sahihi juu ya eneo la wakimbizi, tumewajulisha mamlaka husika za kitaifa juu ya ripoti hizi na kuwaomba watoe msaada wa haraka ikiwa meli hiyo itapatikana katika eneo lake la utafutaji na uokoaji. Hatua ya haraka inahitajika kuokoa maisha. Na zuia majanga zaidi. " 

UNHCR imesema, wakimbizi hao inadaiwa walitoka Cox's Bazar na Tecnaf kusini mwa Bangladesh takriban siku kumi zilizopita, na boti zao zilikuwa zimekwama baharini kwa sababu ya kuharibika injini, kwa zaidi ya wiki moja iliyopita.  

Wakimbizi wanaripoti kwamba chakula na maji vinakosekana kwenye meli kwa siku kadhaa, na abiria wengi ni wagonjwa. 

Waislamu wanaodhulumiwa wa jamii ya Rohingya nchini Myanmar

Eneo la maji la Andaman ni sehemu ya maji ya Bahari ya Hindi. Iko kusini mashariki mwa Ghuba ya Bengal, kusini mwa Myanmar, magharibi mwa Thailand, na mashariki mwa Visiwa vya Andaman na Nicobar nchini India. 

UNHCR imetoa wito kwa serikali mbalimbali kupeleka timu za utafutaji na uokoaji ili kwa haraka kuwaokoa waathirika,  na kusisitiza kuwa, "kuokoa maisha lazima kiwe kipaumbele." 

Ratwater amehimiza kwamba, "nchi zote zinapaswa kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kuwaokoa watu walio katika shida baharini kulingana na majukumu ya kimataifa ya sheria ya bahari, bila kujali utaifa wao au hali yao ya kisheria." 

Aidha Ratwater ameeleza kuwa UNHCR iko tayari kusaidia serikali katika eneo hilo katika siku zijazo kutoa msaada wowote wa kibinadamu na hatua za karantini kwa kadri ya makubaliano ya afya ya umma kwa watu wanaoshuka kutoka katika meli.   

Read Entire Article