PERMISSIONS

Uhalifu mkubwa waripotiwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

1 week ago 26

Hali ya usalama inazidi kuzorota kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ngome kuu ya upinzani dhidi ya vikosi.

Ripoti zinasema kuwa, kumeongezeka visa unyanyasaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ambapo makundi ya waasi na wanajeshi wa Russia wanaosaidia vikosi vya serikali wanahusishwa katika uhalifu huo. Aktharri ya wahanga wa matukio hayo ni raia wa kawaida.

Mauaji ya umati, vitendo vya ubakaji, vijiji kuchomwa na kuteketezwa kwa moto na shambulio la helikopta, ni baadhi ya visa vinavyoripotiwa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Duru za usalama zinathibitisha kuweko ongezeko la visa hivyo katika wiki za hivi karibuni, lakini ni vigumu kwa mashirika ya kutoa misaada kufika eneo hilo. Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, hivi karibuni ililazimika kusitisha shughuli zake za kuondoa mabomu katika eneo hilo.

Wanamgambo wa Kikristo wa Anti-Balaka

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yaliibuka mwaka 2013, baada ya waasi wa Seleka kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo, François Bozizé. Baada ya Rais Mwislamu, Michel Djotodia kuchukua mamlaka, waasi na magaidi wa Kikristo wenye kufurutu ada wa Anti-Balaka walianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya jamii ya Waislamu, ambapo maelfu waliuawa na wengine wengi kuwa wakimbizi.

Umoja wa Mataifa umetuma kikosi maalumu cha kulinda amani nchini CAR kinachojulikana kama MINUSCA ambacho kimefanikiwa kuleta utulivu wa wastani katika nchi hiyo.

Read Entire Article