PERMISSIONS

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 24.02.2021: Dybala, Henderson, Haaland, Silva, Badiashile, Milenkovic

1 month ago 30

Dakika 4 zilizopita

Paulo Dybala

Chanzo cha picha, Twitter/ BBC

Mustakabali wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala kuendelea kuwachezea mabingwa wa ligi ya Serie A, Juventus haujulikani na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuuzwa msimu huu. (Mirror)

Livepool, Manchester United na Tottenham ni miongoni mwa vilabu vinavyomfuatilia Dybala. (Goal)

Tottenham na Borussia Dortmund wanaongoza katika mbio za kumsajili mlinda mlango wa Manchester United Dean Henderson,23. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Reuters

Chelsea inaamini kwamba itamsajili mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20,kutoka Borussia Dortmund majira ya joto. (Eurosport)

Mmiliki wa The Blues Roman Abramovich atampa kocha wa Chelsea Thomas Tuchel kiasi cha pauni milioni 260 kutumia wakati wa dirisha lijalo la usajili, bila kujalli kama klabu itafuzu kwa ligi ya mabingwa. (Tutto Mercato, via Star)

West Ham itasikiliza ofa iliozidi pauni milioni 100 ili kumuachia kiungo wa kati wa England Declan Rice, 22. (Talksport)

Maelezo ya picha,

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel

Manchester united inaweza kupatiwa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Mreno Andre Silva,25, wakati wa dirisha la usajili msimu wa joto. (Sun)

United wataanza mikkati ya kumnunua kwa Silva ikiwa wataamua kutoongeza mkataba wa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani,34. (Metro)

Klabu hiyo ya Ole Gunnar Solskjaer pia ilimfuatilia mlinzi wa Monaco, Mfaransa Benoit Badiashile,19, msimu wa joto uliopita. (Mirror)

Badiashile amesema hajutii kuikatalia United.(RMC Sport,via Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa kati wa Fiorentina, Mserbia Nikola Milenkovic,23, ni pendekezo namba moja anayelengwa na Borussia Dortmund. (Sky Sports German-in German)

Manchester United pia ina hamu ya kutaka kumsajili Milenkovic. (Express)

Arsenal itasikiliza ofa kwa ajili ya kiungo wa kati Reiss Nelson,21, mwishoni mwa msimu. (CBS,via Mirror)

Washika bunduki hao wako kwenye mazungumzo na mchezaji wao kinda Miguel Azeez,18, kuhusu mkataba wa muda mrefu (Sun)

Read Entire Article