PERMISSIONS

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 03.03.2020: Varane, Donnarumma, Bale, Mbappe, Haaland, Hofmann

1 month ago 20

Dakika 3 zilizopita

Mchezaji wa safu ya kati na nyuma Mfaransa Raphael Varane

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa safu ya kati na nyuma Mfaransa Raphael Varane

Real Madrid wako tayari kumuuza mchezaji wao wa safu ya kati na nyuma Mfaransa Raphael Varane kwa Manchester United baada ya kukubali kiungo huyo aliye na umri wa miaka 27, hatasaini mkataba mpya uwanjani Bernabeu. (Manchester Evening News)

Chelsea bado wanafuatilia hali ya kipa wa Italia Gianluigi Donnarumma,22, AC Milan, na huenda wakamnunua ikiwa hatasaini mkataba mpya katika klabu hiyo ya Serie A. (Eurosport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale

Mchezaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 31, ambaye yuko Tottenham kwa mkopo ataishinikiza Real Madrid kuheshimu mwaka wa mwisho wa mkataba wake ambao malipo yake ni £600,000-kwa wiki, hata kama ataachana na mabingwa hao wa Uhispania msimu huu. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Jonas Hofmann

Kiungo wa kati wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Jonas Hofmann, 28, amedokeza Chelsea – inayoongozwa na mkufunzi wake wa zamani Borussia Dortmund Thomas Tuchel – inataka kumsajili. (Ruhr Nachrichten via Mail)

Barca na Atletico Madrid wameagizwa kupunguza mishahara kwa kiwango kikubwa kutokana na jinsi janga la corona lilivyoathiri La Liga. (Sun)

Maelezo ya picha,

Lionel Messi

Mgombea urais wa Barcelona Joan Laporta amesema mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi, 33, ataondoka klabu hiyo ikiwa hatashinda uchaguzi wa Machi 7. Mkataba wa sasa wa Messi unamalizika msimu huu. (Marca)

Dortmund wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Sevilla na Morocco Youssef En-Nesyri, 23, kuchukua nafasi ya Haaland. (Eurosport)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe

Manchester United lazima ” itikise ardhi na mbingu” kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,20, au mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe,22, anasema mlinzi wa zamani wa Red Devils, Rio Ferdinand. (Mirror)

Aston Villa hawajaamua ikiwa watampatia mkataba wa kudumu kiungo wa kati wa Chelsea anayechezea klabu hiyo kwa mkopo Ross Barkley, baada ya mkufunzi Dean Smith kutilia shaka thamani ya mchezaji huku Blues wakiitisha £35m. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Youssef En-Nesyri

Dortmund wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Sevilla na Morocco Youssef En-Nesyri, 23, kuchukua nafasi ya Haaland. (Eurosport)

Badala yake, Villa wanastahili kumsajili kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge,23 – ambaye anahusishwa na klabu ya Birmingham – anasema mshambuliaji wa zamani wa England Emile Heskey. (Birmingham Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kipa wa Leeds United Mfaransa Illan Meslier

Kipa wa Leeds United Mfaransa Illan Meslier, 21, amevutia “baadhi ya klabu kubwa” kutokana na utenda kazi wake mzuri katika Ligi ya Primia msumu huu, anasema ajenti wake. (Yorkshire Evening Post)

Kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 22, ana vigezo vyote vya kuwa mchezaji nyota duniani, kwa mujibu wa mchezaji mwenza wa zamani wa Hammers, Sebastien Haller. (Talksport)

Meneja wa Sheffield United Chris Wilder anasema “hajui” ikiwa ataongoza Bramall Lane msimu ujao, akiongoza kuwa atasalia klabu hiyo ikiwa “itazingatia mpango uliowekwa”. (Yorkshire Post)

Read Entire Article