PERMISSIONS

Tetesi za soka Ulaya Jumanne 14.09.2021: Pogba ,Bellingham, Rice, Werner, Lingard, Bastoni, Kessie

1 week ago 282

Dakika 9 zilizopita

Cristiano Ronaldo na pogba

Chanzo cha picha, Mirror/Twitter

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo na Pogba

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 28, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na PSG na Real Madrid, anelekea kuongeza kandarasi yake katika klabu ya Man United baada ya Cristiano Ronaldo kurudi Old Trafford. (Athletic, subscription required)

Ingeligharimu dau la yuro milioni 100 ama zaidi kwa klabu ya Borussia Dortmund kumruhusu kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 18 Jude Bellingham kuondoka , huku klabu za Manchester City na Liverpool zikidaiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa England.. (Bild – in German)

West Ham, kama Dortmund, pia imemuwekea bei nyota wao . The Hammers inataka sio chini ya £100m kumuuza kiungo wa kati wa England Declan Rice, 22. (football.london)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Declan Rice

Chelsea inajiandaa kumpatia kandarasi mpya kiungo wa England Mason Mount , hatua ambayo huenda ikamfanya mshahara wake kuongezeka hadi £150,000 kwa wiki. (90min)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United na England Axel Tuanzebe, 23, anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo katika klabu ya Aston Villa kuwa wa kudumu.. (Sun)

Bayern Munich inataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na Chelsea Timo Werner, 25, Januari. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Timor Werner

Leicester City ina hamu ya kumsajili kiungo wa Manchester United na England Jesse Lingard. (Fichajes – in Spanish)

Chelsea inaweza kuwanyatia mabeki wa Inter Milan na Itali Alessandro Bastoni 22 na raia wa Slovakia Milan Skriniar (Mediaset – in Italian)

Tottenham imewasilisha ofa ya kumsajili kungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie, 24, ijapokuwa haijulikani iwapo Spurs itawasilisha ombi hilo mwezi Januari au kusubiri kumsaini mchezaji huyo wa Ivory Coast katika uhamisho wa bila malipo mwezi January (Calciomercato, in Italian)

Read Entire Article