PERMISSIONS

'Taliban wa Marekani': John Walker Lindh, mwanajihadi wa Marekani aliyekutana na Bin Laden kabla ya 9/11

1 week ago 24

Saa 8 zilizopita

John Walker Lindh

Chanzo cha picha, Toby Harnden private collection / Polaris

Maelezo ya picha,

John Walker Lindh fue detenido en Afganistán a finales de 2001.

John Walker Lindh alikulia katika familia ya Kikatoliki mjini Mill Valley, kaskazini mwa San Francisco. Hata hivyo, duniani anajulikana kama “Taliban wa Marekani”.

Lindh alikuwa raia wa kwanza wa Marekani kuzuiliwa mwanzo wa kile kilichoitwa “vita dhidi ya ugaidi” iliyotangazwa na Rais George W. Bush baada ya shambulio la Septemba 11, 2001.

Kukamatwa kwake nchini Pakistan, ambapo alikuwa sehemu ya kitengo cha kijeshi kilichokuwa na wageni 75 wanaopigana katika ngome ya Taliban ,kulisababisha ghasia na picha za kijana huyo mwenye ndevu aliyeonekana kuchanganyikiwa zilienea duniani.

“Nilikiri makosa kwamba nilihudumu kama mwanajeshi wa Taliban mwaka jana kuanzia Agosti hadi Disemba.Wakati huo, Nilibeba bunduki na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono.

Nilifanya hivyo kwa hiari nikijua kwamba ni kinyume cha sheria,” Lindh alisema mwezi Julai 2002, baada ya kufikia makubaliano na ofisi wa waendesha mashtaka kuepuka kifungo cha maisha, na badala yake afungwe miaka 20 jela.

Lakini je kijana huyu mdogo wa California alikuaje mwanajihadi na kupata mafunzo ya kijeshi katika kambi inayofadhiliwa na Osama bin Laden?

Kati ya Malcolm X na Osama bin Laden

Licha ya malezi yake ya utotoni katika misingi ya Kikatoliki, Lindh alianza kuvutiwa na Uislamu alipokuwa kijana mkubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Picha za kwanza za Lindh baada ya kukamatwa kwake zillisambaa kote duniani.

Kulingana na baba yake, Frank Lindh, mwanawe akiwa na miaka 12 alivutiwa sana na filamu za Malcolm X, iliyoandaliwa na Spike Lee, zinazoonesha picha ya mahujaji waliokuja Makka.

Kutoka hapo, alianza mchakato wa utafiti na miaka kadhaa baadae alijiunga na dini ya Kiislamu.

“Alikuwa katika njia panda wakati huo. Hakuwa na hakika anaelekea wapi duniani.

Ilionekana kuwa Uislamu na dini ilikuwa njia yake ya kufikia utambuzi wa kiroho.

Kwa hivyo, akiwa na umri wa miaka 17, Lindh alipata ruhusa kutoka kwa wazazi wake kusafiri kwenda Yemen kusoma Kiarabu.

Nana alielezea kuwa kijana huyo alikwenda kwenye taasisi hiyo na kwamba muda mfupi baada ya kusilimu akaamua kujifunza Kiarabu na kuhifadhi Korani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Linsh anaaminika aklibadilika wakati alipokuwa akisoma shule ya Kuran nchini Pakistan.

Kisha alirejea California, ambako alikaa kwa miezi kadhaa kabla ya kuamua kurudi Yemen. Akiwa huko alimuandikia barua baba yake kuomba kama anaweza kwenda Pakistan kuendelea na masomo yake.

Ombi ambalo baba yake aliridhia bila hakusita.

Nchini Pakistan, Lindh alijiunga na chuo cha mafunzo ya kidini mjini Bannu, kaskazini magharibi mwa nchi, ambako alibadilika zaidi.

Bila wazazi wake kujua, mwezi Juni 2001 Lindh aliamua kuvuka mpaka na kuingia nchini Afghanistan.

Kwa usaidizi wa kundi la wanamgambo, alipokea mafunzo ya kijeshi kwa miezi miwili katika kambi ya al-Farouq nchini humo yakifadhiliwa na Osama bin Laden.

Wakati huo, alikutana mara mbili na kiongozi huyo wa al Qaeda, ijapokuwa kulingana na baba yake hakuwa na uhusiano wowote na ugaidi.

“Alikuwa mmoja wa maelfu ya vijana wa Kiislamu ambao kwa miaka kadhaa walijitolea kuhudumu nchini Afghanistan dhidi ya wababe wa kivita wa wakiungwa mkono na Urusi” (wa muungano wa kaskazini), Frank Lindh aliambia BBC katika mahojiano mwaka 2011.

Hata hivyo, Michael Chertoff, ambaye alikuwa mwanasheria mkuu msaidizi wakati wa kesi ya Lindh, hakuamini kijana huyo hakuwa na uhusiano wowote na ugaidi.

“Alienda kupigania serikali ambayo ilikuwa na uhasama na Marekani na ambayo iliunga mkono mashambulio ya 9/11. Sio uhaini haswa, lakini naweza kusema ni binamu wa karibu wa uhaini,” Chertoff aliiambia BBC mnamo 2011.

Mashtaka ya kwanza dhidi ya Lindh yalionyesha kwamba al Qaeda ilipendekeza kufanya shambulio dhidi ya Marekani au Israel lakini kijana huyo alikataa.

Athari ya shambulio la 9/11

Mapema mwezi Septemba 2001, Lindh alikuwa sehemu ya kitengo cha wanajeshi 75 wa kigeni katika eneo la Tahar kaskazini mashariki mwa nchi.

Na hapo ndipo kila kitu kilibadilika.

Baada ya mashambulio ya 9/11, Marekani iliamua kuvamia kijeshi Afghanistan na kuondoa madarakani utawala wa Taliban.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wakati shambulio la kigaidi dhidi ya Marekani, Lindh alikuwa akipigania Taliban nchini Afghanistan.

Wiki kadhaa baada ya mashambulio ya mabomu kuanza nchi humo, kitengo cha wapiganaji wa Lindh kililazimika kurudi nyuma

Wapiganaji hao walitembea kupitia jangwa la Kunduz, ambapo walijisalimisha kwa kikosi cha muungano cha Kaskazini.

Waliahamishwa eneo la Qala-i-Jangi viungani mwa Mazar-e Sarif ambalo lilikuwa likidhibitiwa na Jenerali Abdul Rashid Dostum, mbabe wa kivita wa Afghanistan.

Huku kulifanyika moja wapo ya vita vya umwagikaji damu zaidi nchini Afghanistan, ambavyo vilianza na ghasia za wafungwa wa Taliban zilizomalizika kwa vifo vya mamia na na baadhi ya majenti wa CIA waliokuwa wakiunga mkono muungano wa kaskazini dhidi ya utawala wa Taliban.

Lindh alijeruhiwa mguu lakini yeye pamoja na manusura kadhaa waliamua kukimbilia mafichoni.

Lakini haikuchukua muda Lindh alikamatwa Disemba1, 2001, na kuwekwa kizuizini na vikosi vya Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanzoni mwa Desemba 2001, Lindh alizuiliwa chini ya ulinzi wa vikosi vya Marekani.

Mara baada ya taarifa za kukamatwa kwake kusambaa duniani alibatizwa jina la “Taliban wa Marekani.”

Ni wakati huo wazazi wake walitambua picha yake alipoangaziwa katika taarifa ya habari baada ya kupoteza mawasiliano naye kwa miezi saba.

Lindh alipelekwa Camp Rhino, kituo cha Marekani kilichoko kilomita 190 kusini magharibi mwa Kandahar. Huko, kulingana na maelezo ya baba yake, “walimwacha ndani ya kontena la chuma akiwa bila nguo kwa siku mbili wakati wa usiku katika jangwa la Afghanistan” na bila kutibu majeraha yake.

Huku hayo yakijiri, huko Marekani, kile mama yake, Marilyn Walker, alielezea kuwa “wimbi” lisiloweza kuzuiliwa la utangazaji hasi wa vyombo vya habari.

Wakili Mkuu John Ashcroft alimuelezea Lindh kama “gaidi aliyefunzwa na al- Qaeda kula njama na Taliban kuua raia wenzake.”

Read Entire Article