PERMISSIONS

Sudan yapinga tena hatua ya Ethiopia ya kujaza maji katika bwawa la Renaissance

1 week ago 8

Serikali ya Sudan imezungumzia tishio la kujazwa maji kenye bwawa la Renaissance lnalojengwa na Ethiopia juu ya maji ya Mto Nile na kusema kuwa, Khartoum itatumia nyenzo zote zinazowezekana kwa ajili ya kulinda raia wake.

Sudan imetoa matamshi hayo baada ya kushindwa duru nyingine ya mazungumzo ya kutafuta suluhisho la mgogoro wa ujenzi wa bwawa la maji juu ya Mto Nile huko Ethiopia na kuongeza kuwa, machaguo yote yako mezani kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wa Sudan.

Taarifa iliyotolewa na timu ya mazungumzo ya Sudan imesema, kujazwa maji mengine katika bwawa la Renaissance huko Ethiopia bila ya kuzitaarifu nchi nyingine ni tishio halisi ambalo haliwezi kufumbiwa macho. 

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Ethiopia imepinga mapendekezo yote ya Sudan yaliyoitaka kuruhusu wapatanishi wa kimataifa katika mgogoro wa bwawa la Renaissance.

Wakati huo huo Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ethiopia imetangaza kuwa, haitasaini makubaliano ya aina yoyote yanayoinyima nchi hiyo haki zake za kisheria za kutumia maji ya Mto Nile. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Ethiopia itaendelea na mpango wake wa awamu ya pili ya kujaza maji katika bwawa hilo.

Ujenzi wa Bwawa la Renaissance, Ethiopia

Kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tatu za Misri, Ethiopia na Sudan cha kuainisha haki za kila nchi katika maji ya Mto Nile na suala la kuanza awamu ya pili ya kujaza maji katika bwawa la Renaissance kilimaziliza jana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa bila ya mafanikio yoyote.

Misri na Sudan zinasema ujenzi wa bwawa hilo ambalo limegharimu karibu dola bilioni nne, utapunguza maji ya nchi hizo na hivyo kuvuruga maisha ya mamilioni ya watu. Ethiopia nayo inasisitiza kuwa ujenzi wa bwawa hilo ni muhimu kwa ajili ya kueneza umeme katika nchi hiyo ili kuimarisha sekta ya viwanda na pia kuuza bidhaa hiyo katika nchi za nje.  

Read Entire Article