PERMISSIONS

Rouhani: Makubaliano ya JCPOA hayajadiliki tena, njia pekee ya kuyalinda ni kuondolewa vikwazo vya Marekani

1 month ago 23

Rais Hassan Rouhani amesema, JCPOA ni makubaliano ya kimataifa ya pande kadhaa zinazojulikana wazi na yamethibitishwa na azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na akasisitiza kwamba, makubaliano hayo ya nyuklia hayawezi katu kujadiliwa tena na njia pekee ya kuyalinda na kuyafufua ni kuondolewa vikwazo na Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambapo sambamba na kusisitiza kuwa kuendelea kupotea fursa ya kuyalinda na kuyafufua makubaliano ya JCPOA kunaweza kuifanya hali iwe ngumu zaidi ameongeza kuwa, kupunguzwa hatua kwa hatua uwajibikaji wa Iran kumesababishwa na kujitoa Marekani katika JCPOA na kushindwa nchi tatu za Ulaya pia kutekeleza majukumu yao katika makubaliano hayo; lakini uwajibikaji huo wa Iran utarejea tena katika hali yake ya kawaida mara tu pande zingine katika upande wa pili zitakapotekeleza majukumu yao.

Rais Rouhani amesema, kughairi Iran kutekeleza kwa hiari Protokali ya Ziada kumefanyika kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na bunge na akaongeza kuwa: "Ushirikiano wetu na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki ungali unaendelea na wala hatujajitoa katika JCPOA."

Rais wa Iran ameitaja Ufaransa kama mmoja wa wadau muhimu na akaeleza kwamba, kwa kufuata mtazamo endelevu na kwa ajili ya malengo ya muda mrefu, uhusiano wa Tehran na Paris unaweza kustawi zaidi kwa faida ya mashirikiano ya pamoja ya pande mbili, ya kikanda na kimataifa.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema, kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni jambo la dharura kwa jamii ya kimataifa, na akasisitiza kuendelezwa mazungumzo ya kuwezesha pande zote kurejea kwenye utekelezaji kamili wa makubaliano hayo.../

Read Entire Article