PERMISSIONS

Raisi: Marekani na Wamagharibi zimekanyaga haki za binadamu katika vita vya kulazimishwa

1 week ago 9

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran amesisitiza kuwa, Marekani na Wamagharibi walikanyaga haki za binadamu katika vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na utawala wa Saddam dhidi ya Iran.

Hujjatul-Islam Walmuslimin Sayyid Ibrahim Raisi ameyasema hayo leo katika kongamano la kimataifa la madai ya kisheria na kimataifa ya vita vya Kujihami Kutakatifu lililoanza leo hapa mjini Tehran na akaongeza kwamba, inapasa tuwabainishie walimwengu hatua za Marekani na Wamagharibi za ukiukaji haki za watu katika kipindi cha vita vya kujihami kutakatifu.

Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran ameongeza kuwa, inapasa tuwabainishie watu duniani kote jinsi Wamarekani na Wamagharibi walivyokanyaga haki za binadamu wakati wa vita vya kulazimishwa kwa ajili ya matashi yao na kutokana na uafriti wao.

Utawala wa Saddam ulitumia silaha za kemikali pia katika vita ulizopatiwa na nchi za Magharibi

Sayyid Raisi ameeleza pia kwamba, katika kipindi cha vita vya kulazimishwa, Saddam, dikteta wa zamani wa Iraq alikuwa mwendeshaji, lakini kuna ulazima wa kubainishwa pia nafasi ya washirika wa uhalifu uliofanywa katika zama zile na inapasa kuujuza ulimwengu washirika wa uhalifu uliotendwa katika kipindi kile.

Amesema orodha ya misaada ya kisiasa, ya silaha na ya kifedha iliyotolewa na Wamagharibi kwa Saddam katika kipindi cha vita vya kulazimishwa ni ndefu.

Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Ibrahim Raisi amesisitiza pia kuwa, ikiwa yatafunguliwa mashtaka na kuorodheshwa ndani yake makosa yote ya jinai yaliyofanywa na Marekani na baadhi ya nchi zingine za Magharibi zinazojigamba kutetea haki za binadamu kama Ujerumani na Ufaransa katika zama za Vita vya Kulazimsihwa, faili la mashtaka hayo litakuwa kubwa sana.../

Read Entire Article