PERMISSIONS

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta achagua kuwa mkulima baada ya kustaafu

1 week ago 16

Ikiwa imesalia miezi kumi pekee kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefichua mipango yake baada ya kuondoka mamlakani Agosti 2022 muhula wake utakapotamatika.

Akizungumza akiwa kwenye mkutano na African Green Revolution Forum (AGRF) 2021, Rais wa Kenya amesema kwamba atakuwa akifanya ukulima baada kuondoka madarakani. Uhuru pia alifichua kwamba amekuwa akitamani sana kuwa mwanajeshi tangu alipokuwa mtoto mchanga lakini ndoto yake ilibadilika baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa 2013. "Kusema ukweli, wakati nilipokuwa mtoto mchanga, nilitamani sana kuwa mwanajeshi lakini sasa ukiniuliza nataka nini, nitakwambia nataka kuwa mkulima, kwa sababu hiyo ndio kazi naenda kufanya baada ya kustaafu", amesema kiongozi wa Kenya.

Uhuru amewahakikishia Wakenya kwamba makabidhiano ya madaraka yatafanywa kwa njia ya amani na Rais atakayemrithi.

Akiwa kwenye mkutano na wanahabari Ikulu mwezi Agosti, Uhuru alikanusha madai kwamba, anapanga kuendeleza utawala wake. "Niko tayari kwa uchaguzi na sina mpango wa kusalia afisini muhula wangu ukikamilika," alisema Uhuru Kenyatta.

Mapema mwezi huu, Rais Uhuru Kenyatta aliwachagua maafisa wapya wa tume ya uchaguzi IEBC ambao wameshaidhinishwa na Bunge.

Read Entire Article