PERMISSIONS

Rais wa Afghanistan atoa onyo kwa Taliban kuhusiana na kushupalia kuendeleza vita

1 week ago 9

Rais Ashraf Ghani wa Afghanistan ametoa onyo kwa kundi la Taliban kuhusiana na msimamo wake wa kuendeleza vita nchini humo.

Ashraf Ghani ametoa onyo hilo katika mahojiano na kanali ya BBC na kusisitiza kuwa Taliban haitashinda katika medani ya mapigano na wala haina nguvu na uwezo wa kuipindua serikali.

Pamoja na hayo, Rais wa Afghanistan amekiri kuwa upo uwezekano wa nchi hiyo kutumbukia kwenye lindi la vita vya ndani.

Indhari ya kutokea vita vya ndani nchini Afghanistan inatolewa kwa mara ya kwanza na rais wa nchi hiyo.

Hivi karibuni, Rais Ashraf Ghani alisisitiza kuwa, madamu yuko hai hataruhusu kuundwa serikali ya muda nchini Afghanistan.

Wanamgambo wa kundi la Taliban

Kabla ya hapo, kiongozi huyo alikuwa ameshaeleza pia kuwa, atakabidhi madaraka ya nchi kwa serikali nyingine itakayochaguliwa na wananchi baada tu ya kipindi cha uongozi wa serikali yake ya sasa kitakapomalizika.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Marekani inaingilia masuala ya ndani ya Afghanistan na kulitumia suala la kuundwa serikali ya muda linalopingwa vikali na viongozi wa nchi hiyo ili kuandaa mazingira ya kuiangusha serikali ya Rais Ashraf Ghani.../

Read Entire Article