PERMISSIONS

Rais Mattarella wa Italia alaani mauaji ya Balozi wake DRC

1 week ago 6

Balozi huyo ameuawa mchana wa leo wakati msafara wa Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP, ulipovamiwa na watu wenye silaha mashariki mwa Kongo.

Watu wengine wawili wameuawa pia kwenye uvamizi huo, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kongo katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Meja Guillame Djike. Kwa mujibu wa vyanzo vyengine Balozi Attanasio alikufa kutoka na majeraha sambamba na dereva mmoja na mlinzi mmoja wa msafara huo.

Waziri Mkuu wa Italia, Mario Draghi, ameelezea masikitiko yake makubwa kutokana na mauaji hayo, akisema kuwa jamhuri nzima inaomboleza vifo vya watumishi hao wa umma. Jeshi nchini Kongo linasema linawasaka waliohusika na mauaji hayo.
 

Read Entire Article