PERMISSIONS

Mufti Abubakar Zubeir awataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kuishi bila hofu ya maradhi

1 month ago 15

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali amewasihi Watanzania wote kujenga utamaduni wa kuishi bila ya kuwa na hofu ya maradhi mbalimbali kwani kufanya hivyo ni kujitia katika hatari.

Mufti wa Tanzania amesisitiza kuwa, hofu ni miongoni mwa magonjwa makubwa na hatari mno ambayo hudhoofisha mwili na hatimaye kumfanya mtu aangamie kutokana na ile hofu na wasiwasi aliokuwa nao.

Sheikh Abubabakr Zubeir amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari hapo jana na kubainisha kwamba, jambo la kwanza ambalo Watanzania wanapaswa kulifanya hasa katika kipindi hiki ni kuondoa hofu katika nyoyo zao na kumrejea Mwenyezi Mungu.

Aidha amewasihi Watanzania kumtegemea Mwenyezi Mungu na kufuatia maelekezo na miongozo ya Wizara ya Afya katika kukabiliana na ueneaji wa virusi vya Corona hasa suala zima la usafi.

Mufti Mkuu wa Tanzania mbali na kueleza kwa kirefu madhara ya hofu na kujiepusha na hofu na woga amesisitiza pia, watu wanapaswa kujiepusha la suala la kuwahofisha na kuwatia hofu wenzao.

Rais Joh Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kadhalika amewataka Watanzania kuwa na msimamo na kutokubali kuyumbishwa na kwamba, wananchi wote kila mmoja kwa dini yake, amrejee Mwenyezi Mungu na kumuomba aivushe jamii katika kipindi hiki cha changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya afya.

Tanzania iliacha kutangaza takwimu za maambukizi au vifo vya virusi hivyo mwezi Aprili mwaka jana (2020) baada ya maafisa wa maabara ya taifa kutuhumiwa kutoa matokeo yasiyo sahihi. Aidha Rais John Pombe Magufuli alitangaza Julai mwaka jana kwamba, Tanzania haina tena virusi vya Corona baada ya siku tatu za maombi ya kitaifa.

Read Entire Article