PERMISSIONS

Mtaalamu wa jeni: Kuna uwezekano COVID-19 haikuanzia Wuhan, China

1 week ago 22

Mtaalamu wa jeni amesema, kuna uwezekano kwamba ugonjwa wa COVID-19 haukuanzia katika mji wa Wuhan huko China.

Peter Forster ambayye ni mtaalamu wa jeni na Makamu Mkuu wa Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Cambridge ya Masuala ya Utafiti ameeleza kuwa, dhana kwamba ugonjwa wa COVID-19 ulianzia katika soko la vyakula vinavyovunwa kutoka baharini huko Wuhan ni ya upotoshaji.

Hadi sasa watu milioni 219 wamepatwa na maambukizi ya kirusi cha corona duniani na zaidi ya milioni 4.5 wameuawa na virusi hivyo. 

Mtaaalamu huyo wa jeni kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge ameongeza kuwa, aina za spishi za kirusi cha corona zilizosababisha maambukizi makubwa duniani zikiwemo spishi za Delta na Beta zinaweza kujulikana chanzo chake kulingana na mabadliko yaliyotokea nchini Italia.

Timu ya Forster ilichunguza hifadhi data ya asili ya taarifa za kijenetiki kuhusu virusi zilizochukuliwa katika awamu ya kwanza ya wagonjwa wa COVID-19 kati ya Disemba 2019 na mwezi Machi mwaka 2020. Baadaye timu hiyo ilifanikiwa kugundua kirusi chenye umri mkubwa walichokipa jina la Type A. Timu hiyo ilifikia natija kuwa, kirusi hicho hakikuwa kile kilichogunduliwa awali huko Wuhan na kwamba kilianzia sehemu nyingine na kubadilika kabla ya kuwasili katika mji wa Wuhan. 

Soko la vyakula vya baharini la Wuhan, China  
Read Entire Article