PERMISSIONS

Michezo ya kieletroniki yahimizwa nchini Kenya kwenye kipindi cha virusi vya Corona

1 week ago 13

Kenya yapanua mauzo ya maparachichi nchini China Kenya inapania kupa...nua mauzo ya parachichi katika soko la China ili kuongezea mapato kwa wakulima na wadau wengine kwenye sekta ya uzalishaji wa tunda hilo. Kampuni moja nchini Kenya ya Mofarm Fresh Fruits Exporters, tayari imekuwa ikishirikiana na wakulima wa parachichi kwa kununua mazao yao kwenye soko la China. Ronald Mutie anaripoti kutoka Nairobi. Kenya ililianza kuuza parachichi katika soko la China mnamo mwaka wa 2019, hii ni baada ya Kenya kuzingatia masharti yote ya sokoni kama ilivyotiwa Saini na maraisi Xi Jinping wa China na Uhuru Kenyatta wa Kenya. Kwenye mkataba huo wa kibiashara baina ya mataifa haya mawili, Kenya ilitakiwa kusafirisha parachichi iliyoganda almaarufu frozen avocado kama njia moja ya kudhibiti athari zitokanazo na wadudu . Meneja wa operseheni katika kampuni ya kununua na kusafirisha parachichi katika mataifa ya ulaya ya Mopham fresh fruits exporters Boniface Kimeu Mutungi, anasema soko la China lina faida tele kwa mkulima wa parachichi “Ukilinganisha na soko zingine kama vile Misri, Libya na Dubai, soko la China bei yake iko juu” Bwana Mutungi anasema kwamba soko la China linathamini sana aina moja ya parachichi kutokana na ubora wake “China waliitisha avocado aina ya hass ambayo ngozi yake iko juu, pia wanataka parachichi ambazo zimekomaa” Halikadhalika, teknolojia hutumika pakuwa katika biashara na soko la china ili kuhakikisha bidhaa zinazotumwa kwenye soko hilo la kimataifa zinaafiki viwango hitajika “Hii mashine hapa tunatumia kupima ukomavu na kiwango cha mafuta kwenye parachichi” Mkulima kutoka jimbo la Muranga nchini Kenya Iringo Kamau, anafurahia namna soko la china limewapa faida kama wakulima wa parachichi Tuko kwenye kundi la wakulima 120 tanalima parachichi. Kabla ya kuingia kwenye kampuni ya Mofarm tulikuwa tunateseka sana kwa mambo kama uchukuzi na uuzaji Afisa mkuu mtendaji katika kampuni ya Mofarm fresh fruits exporters Magdaline Njoki, anaweka wazi kwamba idadi ya wakulima wanaokuza zao la parachichi majimboni nchini Kenya inazidi kuongezeka kutokana na faida inayoambatana na kilimo hicho “Mkurungezi mkuu wa Mofarm ameshika huo mwito wa kufundisha wakulima na tumekuwa tukinunua parachichi kutoka Muranga, Nyeri, Nakuru Eldoret na kadhalika” Tangu mwaka 2019, serikali ya China imekuwa ikikuza biashara kati yake na Afrika ikizingatia hasa biadhaa za kilimo badala ya zile za madini kuingia kwenye soko lake. Parachichi kutoka kenya imekuwa ni sehemu ya mpango huo utakaowezesha kupunguza mwanya wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. See More

Read Entire Article