PERMISSIONS

Mapinduzi ya Myanmar: Waandamanaji wakaidi onyo la jeshi

1 week ago 5

Dakika 4 zilizopita

Thousands gather in Mandalay, Myanmar on Monday

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Viongozi wa kijeshi waliipindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Aung San Suu Kyi tarehe 1 Februari

Maelfu ya waandamanaji wameingia kwenye mitaa mbali mbali ya Myanmar katika mopja ya maandamano makubwa dhidi ya mapinduzi ya kijeshi nchini humo.

Biashara zote zimefungwa huku wafanyakazi wakijiunga na mgomo wa jumla, licha ya taarifa ya jeshi kusema kuwa wanahatarisha maisha yao kwa kujitokeza kuandamana.

Polisi wamehangaika kutawanya umati mkubwa watu katika jiji kuu , Nay Pyi Taw, na mitambo ya maji imeonekana ikitumiwa kuwapiga kwa maji maji waandamanaji.

Myanmar imeshuhudia wiki kadhaa za maandamano ya kupinga mapinduzi yaliyofanyika tarehe Mosi Februari.

Viongozi wa Kijeshi waliing’oa madarakani serikali iliyochaguliwa ya Aung San Suu Kyina wamemfunga katika kifungo cha nyumbani, wakimshitaki kwa kumiliki kifaa cha mawasiliano cha radio kinyume cha sheria na kukiuka sheria ya inayohusu majanga asilia.

“Hatutaki junta, tunataka demokrasia. Tunataka kutengeneza hali yetu ya baadae ,” uandamanaji mmoja kwa jina Htet Htet Hlaing, aliliambia shirika la habari la Reuters katika mji wa Yangon.

Unaweza pia kusoma:

Taarifa kutoka katika jeshi iliyosomwa katika televisheni ya taifa , MRTV ilisema kuwa waandamanaji “sasa wanawachochea watu, hususan hisia za vinajana kutumia njia ya makabiliano ambako watapoteza maisha”.

Iliotahadharisha watu dhidi ya “ghasia na machafuko”. Onyo hilo lilisababisha mtandao wa Facebook kuondoa kurasa za mtangazaji kwa kukiuka sera zake za “ghasia na uchochezi ”

Hii inakuja baada ya watu wawili kuuawa katika maandamano siku ya Jumapili-katika maandamano mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa zaidi ya wiki mbili.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jeshi na polisi wakiwatawanya waandamanaji katika mji mkuu Nay Pyi Taw Jumatatu

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wandamanaji walikusanyika katika miji mikubwa, ukiwemo mji wa huu Yangon

Waandamanaji wanadai kumalizika kwa utawala wa kijeshi na wanataka Bi San Suu Kyi aachiliwe huru, pamoja na maafisa wa ngazi ya juu wa chama chake cha National League for Democracy (NLD).

Shinikizo la mataifa ya kigeni dhidi ya viongozi wa kijeshi pia lilmekuwa la hali ya juu. Katika hotuba yake siku ya Jumatatu Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Dominic Raab anatarajiwa kudai Bi Suu Kyi aachiliwe.

Ni yapi matukio ya hivi punde?

Maandamano yanafanyika katika miji yote mikuu ya Myanmar, huku wakipeperusha bendera na kushangilia

Vyombo vya habari nchini huo vimekua vikitweet picha za umati mbali mbali wa waandamanaji kutoka maeneo mbali mbali ya nchi:

Maandamano ya Jumatatu yamepewa jina “22222 Revolution” kwasababu yamefanyika tarehe 22 Februari. Yanalinganishwa na maaandamano ya tarehe 8 Agosti 1988 – yanayofahamika kama mwamko wa 8888 – wakati Myanmar iliposhuhudia moja ya maandamanao ya ghasia zaidi. Jeshi liliwakamata waandamanaji,na kuwaua mamia ya waandamanaji.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Apiga picha akifanya mazoezi bila kujua serikali yake inapinduliwa

Read Entire Article