PERMISSIONS

Mafuriko yauwa zaidi ya watu 80 Sudan

1 week ago 15

Hayo yameelezwa na afisa mmoja nchini humo jana Jumatatu. Msemaji wa baraza la kitaifa la ulinzi wa raia,Andel Jalil Abdelreheem amesema Jumla ya watu 84 wamefariki na 67 wengine wamejeruhiwa katika majimbo 11 kote nchini Sudan tangu msimu wa mvua ulipoanza nchini humo.

Vifo hivyo vimetokana na watu kuzama,kupigwa shoti ya umeme na majumba kuporomoka. Kiasi ya majumba 8,408 pia yamebomoka kabisa na mengine 27,200 yameharibiwa kote nchini Sudan.

Umoja wa Mataifa umekadiria kwamba mvua kubwa na mafuriko yamewaathiri kiasi watu 102,000 tangu mwezi Julai.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya wiki iliyopita ilisema kwamba takriban vijiji 50 vimesombwa na maji Kusini mwa Sudan na kusababisha watu 65,000 wakiwemo wakimbizi kutoka Sudan Kusini waliokuwa wakiishi kambini kuachwa bila makaazi baada ya kambi yao kusombwa.

Read Entire Article