PERMISSIONS

Kwanini serikali ya China inadhibiti makampuni makubwa ya teknolojia?

1 week ago 33

Dakika 5 zilizopita

Jack Ma

Chanzo cha picha, Getty Images

Kila kitu kilikuwa sawa kwa kampuni ya Ali Baba kuanzia uuzaji wa kwanza wa hisa katika masoko ya hisa ya Hong Kong na Shanghai mnamo Novemba 2020 kwa thamani ya dola za Kimarekani bilioni 34.4.

Lakini katika dakika ya mwisho, wasimamizi wa kifedha wa China walisitisha operesheni hiyo kwa sababu ya “wasiwasi kuhusu ushindani” kwenye soko.

Hiyo ni, walikata umeme, wakazima muziki, na kuwarudisha wageni nyumbani.

Matokeo yake ni kwamba mamlaka ilidai marekebisho ya kampuni kubwa zaidi ya biashara na dijiti ya China, na Jack Ma, ambaye zamani alikuwa ishara ya mafanikio ya ujasiriamali nchini humo, alikuwa nje ya macho ya umma kwa miezi kadhaa.

Uamuzi usiotarajiwa ulisababisha athari kubwa kimataifa. Lakini kile labda wachache walifikiria wakati huo ni kwamba ulikuwa mwanzo tu wa serikali kuweka udhibit kwa makampuni makubwa ya teknolojia.

Rais Xi Jinping hivi karibuni alitetea kampeni yake ya kuweka udhibiti mkubwa kwa makampuni katika sekta ya teknolojia kwenye mkutano wa Kamati ya Uendeshaji ya Chama cha Kikomunisti cha China, kulingana na ripoti rasmi za waandishi wa habari.

Chanzo cha picha, Getty Images

Lengo lake, alisema kiongozi huyo wa Wachina, ni “kuzuia upanuzi wa mitaji isiyo ya kawaida” wa kampuni za teknolojia.

Pia alitoa onyo la wazi: atazidisha uchunguzi wake kwa kampuni hizi.

“Utekelezaji wa kanuni hizi zote ni muhimu kabisa kuboresha uchumi wa soko la ujamaa na kukuza ustawi wa kawaida,” Xi alisema.

Dhana ya “ustawi wa kawaida” imekuwa nembo mpya ya serikali, ikisema kuwa ni muhimu kugawanya tena utajiri nchini China na kuhimiza ushindani mkubwa kati ya kampuni.

Walioanguka

Baada ya kusimamishwa kwa mpango wa kutoa hisa za Alibaba, serikali iliweka vizuizi kwa viboreshaji vingine vya teknolojia katika maeneo tofauti kama biashara ya elektroniki, usafirishaji, programu kwa ajili ya huduma za kibenki, michezo ya video au kampuni za elimu mtandaoni

Kampuni kubwa ya biashara ya mtandaoni, Alibaba (ambayo pia ni sehemu ya himaya iliyoanzishwa na Jack Ma) ilitozwa faini ya dola bilioni 2.8 mnamo Aprili, faini kubwa zaidi katika historia ya nchi hiyo, baada ya uchunguzi kubaini kuwa kampuni hiyo “ilitumia vibaya nafasi yake kuu katika soko. “

Chanzo cha picha, Getty Images

Vigogo wengine ambao wamekuwa sehemu ya wimbi hili jipya la vizuizi vilivyowekwa na serikali ni: Tencent (internet conglomerate), Meituan (usambazaji wa chakula), Pinduoduo (biashara ya mtandaoni), Didi (sawa na Uber), Full Truck Alliance (usafirishaji na kusambazaji), Kanzhun (ajira), kampuni za elimu mtandaoni kama Huduma za elimu binafsi au Mafunzo baada ya elimu ya msingi na sekondari.

Katika taarifa tatu tofauti za umma, Alibaba, Didi na Meituan wamesema kuwa watashirikiana na mamlaka.

Moja ya kesi za mwisho zinazojulikana ilikuwa ile ya mtengenezaji wa gari la umeme BYD. Kampuni hiyo ilipanga kuuza hisa za kitengo chake cha kutengeneza chip, lakini shughuli hiyo ilisitishwa kwa sababu ya “uchunguzi wa mamlaka za udhibiti.”

Chanzo cha picha, Getty Images

Ingawa kila kesi ni tofauti, hoja zinazotumiwa na Beijing kuhalalisha maamuzi yake zinahusu pande mbili: kudhibiti ukiritimba na “kulinda usalama” wa mtumiaji wa taarifa.

Katika muktadha huu, sheria ilipitishwa hivi karibuni ambayo inaweza kuhitaji kusimamishwa au kufutwa kwa programu ambazo ni “haramu” zinashughulikia “data nyeti” binafsi

Mipango ya mwaka 2025 ikoje?

Serikali ya China imeweka wazi mpango wa miaka mitano unaoelezea kanuni kali katika uchumi wake wote.

Mwandishi wa BBC wa Biashara wa Singapore Peter Hoskins anaelezea kuwa sheria mpya huenda mbali zaidi ya sekta ya teknolojia, pamoja na mambo kama usalama wa kitaifa na ukiritimba wa biashara.

Mpango wa Beijing unaweka katika waraka kwamba sheria zitaimarishwa katika “maeneo muhimu” kama sayansi na uvumbuzi wa kiteknolojia, utamaduni na elimu.

Kulingana na serikali, njia hii mpya itaweka kanuni mpya ambazo zitajumuisha maeneo kama “fedha za mtandao, ujasusi bandia, data na teknolojia ya kompyuta .”

China inaonekana kusonga mbele haraka sana, angalau kutoka kwenye udhibiti wa kukera dhidi ya wakuu wa tasnia ya teknolojia katika miezi ya hivi karibuni kumebainisha.

Read Entire Article