PERMISSIONS

Kwanini ngombe wanafunzwa kwenda chooni Ujerumani?

1 week ago 18

Dakika 6 zilizopita

Корова

Chanzo cha picha, FBN

Maelezo ya picha,

Ngombe huko Ujerumani hufundishwa kwenda kwenye choo ili kusaidia kupunguza athari ya ongezeko la joto.

Wanasayansi katika Taasisi ya Baiolojia ya Wanyama huko Dummersdorf wameonyesha kuwa ngombe wanaweza kufundishwa kutumia choo.

Huu utakuwa mchango mkubwa katika vita dhidi ya ongezeko la joto duniani, waandishi wa utafiti huo wanaamini.

Wakati ngombe wanakwenda chooni mahali popote walipo, amonia katika mkojo wao humenyuka na mchanga kuunda gesi ya nitrous oksidi, ambayo ina athari zake katika ongezeko la joto.

Ufugaji unajumuisha karibu 10% ya gesi zote zilizotolewa angani na shughuli za kibinadamu na kuchangia katika ongezeko la joto duniani.

Utafiti huo ulihusisha ngombe 16, ambapo choo kiitwacho ‘MooLoo’ kilijengwa kwenye shamba linalomilikiwa na taasisi hiyo, na mkojo haukutumwa kwa ajili ya usindikaji.

Chanzo cha picha, FBN

Maelezo ya picha,

Robo ya idadi ya ngombe walitumia choo kilichotengenzwa, amesema mtafiti mmoja

Ngombe walichukuliwa kwa zamu kupelekwa chooni na kupewa huduma maalum kama zawadi ikiwa watakojoa, kisha tabia zao zikafuatili

Ikiwa ngombe alienda chooni akihitaji kujisaidia, alipewa tena huduma maalum, na ikiwa alienda choo mahali pengine, alimwagiwa maji kwa sekunde tatu.

Katika hatua ya mwisho ya jaribio hilo la utafiti, umbali kutoka kwenye uwanda walipowekwa ngombe hadi kwenye choo uliongezeka.

Baada ya mafunzo ya siku kumi, ngombe 11 kati ya 16 walianza kwenda chooni peke yao katika 75% ya visa vilivyofuatiliwa, wakiwa na akili zaidi kuliko watoto wa kibinadamu.

“Walichukuliwa haraka sana baada ya kukojoa mara 15 hadi 20,” alisema biolojia wa New Zealand Lindsay Matthews wa Chuo Kikuu cha Auckland, ambaye alishiriki katika utafiti huo.

Wanasayansi wanakadiria kuwa kuanzishwa kwa vyoo kama hivyo kutasaidia kukusanya hadi 80% ya mkojo wa ngombe na kupunguza gesi amonia angani kwa asilimia 56, bila kusahau ukweli kwamba wanyama watajisikia vizuri kuishi kwenye mabanda yaliyo safi.

Maelezo ya video,

Bioethanol:Mafuta yatokanayo kwa mimea yanayoweza kuzuia athari za tabia nchi

Read Entire Article