PERMISSIONS

Kutana na jamii ya watu nchini Ghana ambao Mbwa na Paka ni kitoweo kizuri

1 week ago 26

Dakika 5 zilizopita

Mbwa na Paka

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa watu wengi wanyama wa kufugwa majumbani ni marafiki ndani ya nyumba, lakini baadhi ya Waghana huwatumia wanyama paka na mbwa kama chakula maalum.

”Joseph” jina maarufu la nyama ya paka nchini Ghana.

Watu wa mkoa wa Volta nchini humo wanatazama nyama ya paka iitwayo ”joseph” kama chakula maalum

Haijulikani kwa nini nyama ya paka imepewa jina Joseph, lakini kwa watumiaji wa nyama hii wanasema ni nyama yenye ladha tamu.

Matumizi ya nyama ya paka kwa watu wa Volta yanafahamika miongoni mwa raia wa Ghana, mpaka kuna wakati watu hupenda kuwatania kuwa hii ni sababu kubwa kwa paka kuwa wachache katika eneo hilo la Ghana.

Lakini walaji wa paka huwatunza paka hawa kwa ajili ya paka, kama vile wanavyofuga kuku, mbuzi au ng’ombe.

Nyama ya paka hupikwa kwa supu yenye pilipili, sambamba na chakula kiitwacho Gari au eba.

Nyama hiyo huandaliwa kwa supu kwa ajili ya kuuzwa mitaani.

Katika maeneo ya kaskazini mwa Ghana, jamii ya Frafra na Dagaaba ni makabila mawili maarufu wanaokula nyama ya mbwa.

Makabila haya huwa na michezo ya kikabila ambayo mshindi wa mashindano hurudi nyumbani na zawadi ya mbwa.

Wala mbwa hutembelea soko la mbwa liitwalo Bolga, ambapo watu huuza nyama ya mbwa.

Kwa watu hawa, mbali na maoni hasi kuhusu nyama ya mbwa, wanaamini kuwa hakuna haja ya kubagua kuhusu nyama gani wanakula na wengine wanakula nyama gani.

Kwa upekee wa nyama hii, wakati mwingine, huandaa nyama ya mbwa kwenye sherehe za harusi.

Hatari ya kupata kichaa cha mbwa, kifua kikuu kutokana na matumizi ya nyama ya mbwa na paka

Wataalamu wa masuala ya afya wanatahadharisha kuhusu hatari ya kupata maradhi ya kichaa cha mbwa kwa kula nyama ya mbwa mwenye maradhi.

Wakati huohuo, madaktari wanatahadharisha kuwa paka na mbwa husababisha maradhi ya kifuakikuu kwa watumiaji wa nyama hizo.

Lakini tahadhari hizi wala haziwazuii watu kula nyama hii inayodaiwa kuwa tamu.

Wanaharakati wa haki za wanyama watoa wito wa kupiga marufuku ulaji wa wanyama hao

Mwanaharakati wa kimataifa wa haki za wanyama, Natasha Choolun, wiki hii ameitaka serikali ya Ghana kupiga marufuku ulaji wa nyama ya paka na mbwa.

”Mbwa na paka si chakula, bali ni marafiki waaminifu tunaopaswa kuwatendea wema na kwa kuwaheshimu, si kwa kuwakatili na kuwala” alisema.

Hoja hiyo imepokelewa kwa namna mchanganyiko, lakini kwa ujumla ulaji wa nyama hii kunatoa maana kwa msemo usemao ”nyama ya mtu mmoja yaweza kuwa sumu kwa mwingine.”

Hivyo basi,kama unataka kujaribu kula nyama ya paka au mbwa, tembelea Ghana.

Nchi za Kiafrika ambazo baadhi ya watu wake wanakula paka na mbwa

Wakati baadhi ya nchi Afrika hula nyama ya mbwa, nchi nyingine kama Uganda huwakamata watu wanaowaua mbwa kwa ajili ya kitoweo.

Lakini nchi nyingine kama Ghana wanakula nyama ya mbwa.

Nchini Nigeria, watu wa Calabar, jimbo la Cross River na wengine kutoka jimbo la Ondo hula nyama ya mbwa.

Nchi jirani ya Liberia pia hula mbwa.

Nchi nyingine kama DRC, pia ina makundi ya jamii fulani yanayokula nyama ya mbwa.

Read Entire Article