PERMISSIONS

Korea Kaskazini: Wanadiplomasia wa Urusi waondoka nchini humo kwa kutumia 'mkokoteni'

1 month ago 34

Dakika 4 zilizopita

KUndi hilo la wanadiplomasia wa Urusi linaloshirikisha watoto lilijisukuma kwa zaidi ya kilomita moja katika reli

Chanzo cha picha, Russian Foreign Ministry/Facebook

Maelezo ya picha,

KUndi hilo la wanadiplomasia wa Urusi linaloshirikisha watoto lilijisukuma kwa zaidi ya kilomita moja katika reli

Kundi la wanadiplomasia wa Urusi na familia zao wameondoka kwa njia isiyo ya kawaida nchini Korea Kaskazini wakiwa wanasukuma mkokoteni kwa mikono kwasababu ya hatua kali zilizowekwa kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona.

Kundi la watu wanane lilisafiri kwa treni na pia basi na baada ya hapo wakalazimika kuchukua mkokoteni na kuanza kuusukuma wenyewe umbali wa takriban kilomita 1 kupitia njia ya treni hadi mpaka wa Urusi.

Korea Kaskazini imefunga njia nyingi za usafiri wa abiria kama njia moja ya kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Nchi hiyo inasisitiza kwamba bado haijawahi kuthibitisha visa vya maambukizi ya ugonjwa huo lakini waangalizi wamekanusha madai hayo.

Tangu mapema mwaka jana treni na magari ya kukokotwa yamekatazwa kuingia au kuondoka nchini humo.

Ndege nyingi za kimataifa pia zilipigwa marufuku.

Wanadiplomasia wa Urusi hivyo basi wakawa wamebaki na machaguo kidogo ya njia za usafiri.

“Kwasababu mipaka imefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na usafiri wa abiria kusitishwa, imechukuwa muda mrefu na safari ngumu kufiki nyumbani,” Waziri wa Urusi wa Mambo ya Nje amesema hivyo katika ujumbe wa Facebook.

Picha zilizotolewa na wizara zimeonesha wanadiplomasia hao wakisukuma mikokoteni walioweka mabegi yao licha ya hali ya hewa ambayo ni baridi.

Maelezo ya video,

mkokoteni

Pia walionekana wakisherehekea wakati wanavuka mpaka kuingia Urusi.

Kundi lillokuwa likisafiri lilijumuisha mtoto wa miaka 3 wa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu, ambalo lilikuwa limesafiri kwa saa 32 kwa kutumia treni na saa mbili kwa basi kutoka Pyongyang hadi mpaka wa Urusi.

Na kisha kundi hilo likasafiri kwa basi hadi uwanja wa ndege wa Vladivostok.

Hatua zilizowekwa na Pyongyang za kukabiliana na ugonjwa wa corona zimeathiri usafiri na ufikiaji wa huduma za msingi.

Pia vikosi zaidi vimepelekwa katika maeneo ya mpakani chini ya maagizo ya kuzuia chochote chenye uwezekano wa kusambaza virusi vya corona.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, wanadiplomasia wengi wa kigeni wameondoka nchini humo na balozi za nchi za magharibi pia zimefungwa.

Wasafiri wengi walivuka mpaka na kuingia China, ingawa kulikuwa na ndege moja tu Machi mwaka jana ya kuelekea Vladivostok iliyokuwa imebeba wanadiplomasia kutoka Ujerumani, Urusi, Ufaransa, Uswizi, Poland, Romania, Mongolia na Urusi.

Read Entire Article