PERMISSIONS

Kifaa kilichotengenezwa kwa ajili ya kufichua jinsia chalipuka na chamuua mwanaume

1 week ago 9

Dakika 5 zilizopita

Picture of Christopher Pekny, taken from his Facebook page

Chanzo cha picha, Facebook

Maelezo ya picha,

Kaka yake Christopher Pekny Peter ameiita ajali hiyo “kituko kikubwa”

Mwanaume mmoja kutoka New York amefariki baada ya kifaa alichokuwa akikitengeneza kwa ajili ya kutumiwa katika sherehe ya kutambulisha jinsia kulipuka , kwa mujibu wa polisi.

Christopher Pekny, mwenye umri wa miaka 28, alikuwa akitengeneza kifaa katika mji wa Liberty wakati kilipolipuka Jumapili mchana.

Polisi inasema mlipuko huo huo ulimuua Pekny na kumjeruhi kaka yake Michael Pekny, mwenye umri wa miaka 27, ambaye alipelekwa hospitalini.

Sherehe za kutangaza jinsia ni sherehe ambapo wazazi hutangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kike ama wa kiume.

Polisi hawakuelezea ni kifaa cha aina gani lilichosababisha mlipuko. Polisi katika jimbo la New York na kitengo chake cha kulipua mabomu wanachunguza tukio hilo..

Msemaji wa pilisi ya jimbo ameliambia gazeti la New York times kuwa kifaa hicho kilikuwa na muundo wa bomba, lakini hakutoa maelezo zaidi. told the New York Times

Akizungumza na gazeti hilo, kaka yake mkubwa marehemu Pekny, Peter Pekny Jr, alielezea kile kilichotokea kama tukio la “kituko kikubwa kuliko vituko vyote ambavyo unawahi kuvifikiria “. Hakujua ni nini kilichosababisha kifaa hicho kulipuka.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kifo hicho ni cha kwanza cha hivi karibuni miongoni mwa vifo vinavyohusiana na sherehe za kutangaza jinsia katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa kawaida sherehe hizi huhusisha michezo ya kubashiri, huku tukio kubwa la ” kufichua jinsia ” likiambatana na kulipua fataki na moshi wa grunedi za rangi.

Lakini sherehe kubwa kadhaa za aina hii zimekuwa zikienda kombo, hata kusababisha vifo.

Mwnaume mmoja kutoka Michigan alikufa mapema mwezi huu baada ya kuumizwa na chuma chenye makali kutoka kwenye “aina ndogo ya chuma cha bomba ” kufyatuliwa wakati wa sherehe ya kumpatia mama zawadi za mtoto mtarajiwa al maarufu baby shower, polisi ilisema.

Sherehe nyingine mbili za kufichua jinsia ya mtoto zilitajwa kuwa chanzo cha moto uliowaka mbugani katika jimbo la California mwezi Septemba 20202, na Arizona mwezi Aprili 2017.

Moto wa El Dorado katika jimbo la California uliteketeza zaidi ya hekari 19,000 , ukachoma nyumba, na kuwalazimisha maelfu kuzikimbia nyumba zao.

Read Entire Article