PERMISSIONS

Jumatano, Septemba 15, 2021

1 week ago 15

Leo ni Jumatano tarehe 8 Mfunguo Tano Safar 1443 Hijria sawa na Septemba 15 mwaka 2021 Milaadia.

Miaka 200 iliyopita yaani tarehe 15 Septemba 1821, nchi za Nicaragua, Honduras, el-Salvador, Guatemala na Costa Rica zilijitangazia uhuru kutoka kwa Uhispania. Baada ya Napoleone Bonaparte mtawala wa Kifaransa kuikalia kwa mabavu Uhispania na kudhoofika serikali ya kijeshi ya Madrid, nchi kadhaa za Latin America zikiwemo Nicaragua, Honduras, el-Salvador, Guatemala na Costa Rica zilijitangazia uhuru. Baada ya nchi hizo tano kujitangazia uhuru ziliunda Muungano wa Amerika ya Kati. Baada ya muungano huo kuvunjika mwaka 1838, nchi wanachama kila moja ilianza kujitawala na kujiendeshea mambo yake yenyewe.

Siku kama ya leo miaka 63 iliyopita, kwa mara ya kwanza katika elimu ya tiba, viligunduliwa virusi vinavyosababisha maradhi hatari ya trakoma yaani mtoto wa jicho. Pamoja na kugunduliwa virusi hivyo yapata miaka kadhaa iliyopita, hadi sasa maelfu ya watu hukumbwa na hali ya upofu duniani, kutokana na maradhi hayo. Virusi hivyo viligunduliwa na madaktari wawili wa Kiingereza.

Na siku kama hii ya leo miaka 22 iliyopita sawa na tarehe 24 mwezi Shahrivar mwaka 1378 Hijria shamsiya, alifariki dunia kwa maradhi ya moyo Dakta Abdulhussein Zarinkub mwanahistoria na mtafiti mashuhuri wa Kiirani. Dakta Abdulhussein alizaliwa mwaka 1301 Hijria Shamsiya katika mji wa Burujerd magharibi mwa Iran. Mwaka 1327 Hijria Shamsiya Dakta Zarinkub alitunukiwa shahada ya digrii katika taaluma ya historia na baadae akaendelea na masomo yake katika taaluma hiyo na kutunikiwa shahada ya udaktari. Mbali na historia msomi huyo wa Kiirani alipenda sana masomo ya fasihi ya lugha ya Kifarsi na irfani ya Kiislamu. Aidha aliandika vitabu na makala nyingi na moja kati ya vitabu vyake ni kile alichokiita "Alfajiri ya Uislamu."

Dakta Abdulhussein Zarinkub
Read Entire Article