PERMISSIONS

Jinsi Saudi Arabia inavyohusika katika mzozo wa Jordan

1 week ago 12

Dakika 7 zilizopita

A frame maker in a frame shop displays pictures of King Abdullah II bin Al-Hussein king of Jordan, in Amman, Jordan, 4 April

Chanzo cha picha, EPA

Maafisa wa Saudi Arabia wamepinga vikali madai kwamba nchi yao ilihusika katik ajaribio la mapinduzi Jordan.

Siku ya Jumamosi mwanafalme maaruufu aliyekuwa mtawala mtarajiwa , Hamzah aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa tuhuma za kuhujumu usalama wa kitaifa baada ya kuhudhuria mikutano ya kijamii ambapo Mfalme Abdullah, ndugu yake wa kambo, alikosolewa hadharani.

Mwanamfalme Hamzah wakati huo aliwasilisha kanda mbili za video kwa BBC, akitaja nchi yake kuwa fisadi na isiyokuwa na uwezo akiongeza kwamba watu wanaogopa kuzungumza kwa kuhofia kuchukuliwa hatua na vikosi vya usalama.

Mzozo huo umetulia baada ya mjomba wa Mfalame kuingilia kati, lakini kumekuwa na minong’ono kuhusu jukumu la Saudi Arabia katika mzozo huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Faisal bin Farhan, alizuru mji mkuu wa Jordan, Amman akiwa na ujumbe wake kama ishara ya “kumuunga mkono Mfalme wa Abdullah wa Jordan na serikali yake”. Hii wanasema, ilikuwa hatua ya kuonesha msimamo wa Saudia Arabia kuhusu suala hilo na kupuuza madai yanayoashiria nchi hiyo ilikuwa na njama ya kudhoofisha jirani yake ni “upizi mtupu”.

Saudi Arabia inahusika vipi?

Wakati mzozo ulipofikia kilele wikendi iliyopita, Maafisa wa Jordan walisema mashirika yao ya usalama yamekuwa yakaifuatilia miendo ya Mwanamfalme Hamzah na maafisa wengine kadhaa kwa muda. Walizungumzia watu wasiojulikana “kutoka nje” ambao wamekuwa wakijihusisha na kile wametaja kuwa njama ya njama ya kudhoofisha nchi na familia tawala ya Hashemite – madai yaliyokataliwa na Mwanamfalme Hamzah.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mtengenezaji fremu za picha akionesha picha ya Mfalme Abdullah mjini Amman

Kilichojitokeza katika mzozo huo ni mambo mawili tofauti. Kwanza Mwanamfalme Hamzah, Mwana wa mkubwa wa kiume wa Mfalame marehemu Hussein, aliyekosana na wakuu wa usalama alipokutana na na viongozi wa kijamii hivi karibuni. Wengine waliohusika ni ni maafisa wanaodaiwa kuwa na ufungamano na nchi nyingine moja.

Mmoja wa viongozi mashuhuri waliyekamatwa Jumamosi ni Bassem Awadallah,Mkuu wa zamani wa mahakama ya kifamle ambaye sasa ni mshauri wa Mnamfalme Mohammed bin Salman. Ana urai pacha wa Saudia na Jordan na anaonekana kuwa na msimamo wa kadri katika makongamano ya Saudi Araia ya masuala ya uwekezaji.

Gazeti la Washington Post liliripoti kuwa waziri wa mambo ya nje wa Saudia na ujumbe wake walizuiliwa kuondoka Jordan hadi watakapoandamana na Bassem Awadallah kwenda Riyadh. Ripoti ambayo maafisa wa Saudi Arabia wamesema sio ukweli.

Bassem Awadullah ana ushawishi mkubwa kimataifa, ikiwa ni pamoja na uhusiano wa karibu na Mwanamfalme na kiongozi wa Milki za Kiarabu UAE, Mwanamfalme Mohammed bin Zayed.

Ameripotiwa kuhusika katika mkakati wa ununuzi wa ardhi wa Palestina unaoungwa mkono na UAE-karibu Jerusalem.

Saudi Arabia na Jordan, japo zinatofautiana pakubwa kiuchumi, zina uhusiano wa kihistoria wa muda mrefu.

Kwa miongo kadhaa nchi hizi mbili zimekuwa na uhusiano ambao umetokana na ufungamano wa kijamii katika mipaka yao ya pamoja jangwani.

Read Entire Article