PERMISSIONS

Jinsi mauaji ya halaiki yalivyotekelezwa katika mji mtakatifu wa Ethiopia

1 month ago 25

Dakika 9 zilizopita

An aerial view of Our Lady Mary of Zion Church and Aksum in Ethiopia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aksum ni mji alikozaliwa Malkia wa Sheba anayezungumziwa katika Biblia

Mapigano ya vikosi vya Eritrea kaskazini mwa eneo la Tigray nchini Ethiopia yamesababisha mauaji ya mamia ya watu eneo la Aksum kwa zaidi ya siku mbili mnamo mwezi Novemba, walioshuhudia wamesema.

Mauaji ya halaiki ya Novemba 28 na 29 huenda yakachukuliwa kuwa uhalifu dhidi ya binadamau, shirika la Amnesty International limesema katika ripoti yake.

Walioshuhudia wameilezea BBC kwamba namna miili ya walio fariki dunia ilivyosalia bila kuzikwa mitaani kwa siku kadhaa huku mingine ikiliwa na fisi.

Ethiopia na Eritrea, ambazo zote zimekanusha uwepo wa wanajeshi wa Eritrea katika eneo la Tigray, hazijasema lolote.

Tume ya Haki za Binadamu nchini Ethiopia imesema kuwa taarifa hizo zinastahili kuchukuliwa kwa uzito mkubwa na kwamba inachunguza madai hayo.

Mapigano yalianza Novemba 4, 2020 wakati serikali ya Ethiopia ilipoanzisha mashambulizi dhidi ya chama cha eneo cha TPLF baada ya wapiganaji wake kuchukua kambi za jeshi la serikali eneo la Tigra.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Novemba 30 aliambia bunge kuwa, “hakuna hata raia mmoja aliyeuawa” wakati wa operesheni hiyo.

Lakini walioshuhudia wameelezea vile walivyoanza kuzika miili ya baadhi ya raia ambao hawakuwa na silaha waliouawa na wanajeshi wa Eritrea – wengi wao wakiwa ni wavulana na wanaume waliopigwa risasi mitaani au wakati wanavamia nyumba hadi nyumba.

Chanzo cha picha, Amnesty/Maxar Technologies

Maelezo ya picha,

Picha za setilaiti zikionesha ushahidi wa hivi karibuni wa makaburi katka kanisa la Arba’etu Ensessa , ambako mazishi ya jumla yaliripotiwa kufanyika

Taarifa za shirika la Amnesty zimesema kuwa picha zilizochukuliwa kwa juu kwa satelaiti kuanzia Desemba 13 zinaonesha maeneo ya ardhini yenye makaburi ya hivi karibuni katika makanisa mawili eneo la Aksum, mji wa kale unaochukuliwa kuwa mtakatifu na Wakiristo wa Kiothodoksi.

Kukatishwa kwa mawasiliano na kuzuiwa kufikiwa kwa eneo la Tigray kumesababisha kutopatikana kwa taarifa kutoka eneo hilo.

Katika eneo la Akusum, mitandao ya simu na umeme ilikatishwa siku ya kwanza ya mapigano.

Unaweza pia kusoma:

Mji wa Aksum ulitekwa namna gani?

Kurushwa kwa mabomu na vikosi vya Ethiopia na Eritrea hadi magharibi mwa Aksum kulianza Alhamisi Novemba 19, kulingana na watu wa mji huo.

“Shambulio hilo liliendelea kwa saa tano bila kusita. Watu waliokuwa makanisani, kwenye migahawa, mahoteilini na maeneo ya makazi wakafariki dunia.

Hakukuwa na kikosi chochote ambacho kilijibu shambulio hilo na badala yake lilikuwa linalenga raia moja kwa moja,” mkaazi wa eneo la Aksum amezungumza na BBC.

Map

Shirika la Amnesty limekusanya taarifa na ushahidi chungu nzima unaoelezea vile mabomu yalivyokuwa yanaendelea kurushwa dhidi ya raia usiku ule.

“Kulikuwa na mauaji mengi yaliyotekelezwa nyumba hadi nyumba,” mwanamke mmoja amezungumza na kundi la haki za binadamu.

Kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kwamba vikosi vya Ethiopia and Eritrean vilitekeleza “uhalifu wa kivita katika uvamizi wake kutaka kuchukua udhibiti wa eneo na Aksum”, Deprose Muchena wa shirika la Amnesty amesema.

Kilichosababisha mauaji hayo ni nini?

Ushahidi uliopatikana unaonesha kuwa vikosi vya Ethiopia vilikuwa katika eneo la Aksum – na wanajeshi wa Eritrea walikuwa wamesonga mbele eneo la mashariki mwa mji wa Adwa.

Aliyeshuhudia amezungumza na BBC na kuelezea vile wanajeshi wa Ethiopia walivyovamia na kupora benki katika mji huo wakati huo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watu wa Tigray wameachwa katika hali ya kutegemea misaada ya kibinadamu

Inasemekana kwamba vikosi vya Eritrea vilirejea wiki moja baadaye.

Mapigano ya Novemba 28, Jumapili, yalisababishwa na mashambulizi dhidi ya kundi la watu maskini waliopendelea wapiganaji wa TPLF, kulingana na ripoti ya Amnesty International.

Kati ya wanaume 50 na 80 kutoka eneo la Aksum walilenga eneo la Eritrea katika kilima asubuhi hiyo.

Mwanamume mmoja, 26, aliyeshiriki shambulizi hilo ameelezea shirika la Amnesty kwamba: “Tulitaka kulinda mji wetu kwahiyo tukajaribu kuutetea dhidi ya wanajeshi wa Eritrea… walijua namna ya kupiga risasi na walikuwa na redio, mawasiliano… Mimi sikuwa na bunduki, yangu ilikuwa fimbo tu.”

Je Vikosi vya Eritrea vilijibu vipi?

Bado haijafahamika mapigano hayo yalichukua muda gani lakini mchana ule, malori ya Eritrea yaliingia eneo la Aksum, taarifa ya Amnesty imesema.

Walioshuhudia wanasema wanajeshi wa Eritrea walianza kupiga risasi raia wasiokuwa na hatia kiholela hasa wanaume na wavulana ambao walikuwa wamejitokeza barabarani – na yakaendelea hadi usiku.

“Mimi nitasema walikuwa wanalipiza kisasi,” kijana mmoja amezungumza na BBC. “Walimuua kila waliemuona. Kama ulifungua mlango wako, walikuwa wanatafuta wanaume na kuwauwa na ikiwa ulikataa walipiga mlango wako kwa risasi na kuingia kwa nguvu.”

Alijificha katika baa moja na kushuhudia mwanamume aliyepatikana akiuawa na wanajeshi wa Eritrea huku akiwa anawaomba wasimuue: “Alikuwa akiwaambia: ‘Mimi ni raia, ninafanya kazi benki.'”

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Walioshuhudia wanasema barabara za Aksum zilkuwa zimetapakaa miili ya watu waliouawa

Ni watu wangapi waliouawa?

Walioshuhudia wanasema kwamba wanajeshi wa Eritrea hawakuruhusu yeyote kukaribia miili ya waliouawa mitaani na pia ikiwa ungejaribu kukiuka hilo wangekupiga risasi.

Mwanamke mmoja ambaye mpwa wake alikuwa na umri wa miaka 29 na 14 aliuawa, amesema kwamba barabara zilikuwa zimejaa miili ya watu”.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mengi kati ya mazishi yaliripotiwa kufanyika katika kanisa la Aksum la Arba’etu Ensessa

Shirika la Amnesty limesema kwamba baada ya wazee kuingilia kati na wanajeshi wa Ethiopia, mazishi ya waliouawa yakaanza kufanyika huku wengi wakizikwa Novemba 30 baada ya watu kupeleka miili hiyo makanisani – ikiwa imerundikana hata 10 kwa kutumia mkokoteni mmoja uliosukumwa kwa farasi au punda.

“Naweza kusema takriban raia 800 waliuawa katika mji wa Aksum”, raia mmoja amesema.

Read Entire Article