PERMISSIONS

Jeshi la Afghanistan lasema limeua wanachama 104 wa Taliban

1 week ago 10

Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limewaua wanachama zaidi ya 100 wa kundi la Taliban ndani ya saa 24.

Katika taarifa ya jana Jumanne, wizara hiyo imesema mbali na wanachama 104 wa Taliban kuuawa, wengine 68 wamejeruhiwa katika operesheni kadhaa za Jeshi la Taifa la Afghanistan (ANA).

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Afghanistan imeongeza kuwa, operesheni hizo zimefanyika katika mikoa ya Ghazni, Zabul, Herat, Farah, Badghis, Faryab, Balkh, Helmand, Badakhshan na Kandahar.

Hata hivyo taarifa hiyo haijaashiria kuhusu kuuawa au kujeruhiwa wanajeshi wa Afghanistan katika operesheni hizo.

Wapiganaji wa kundi la Taliban

Katika miezi ya karibuni, shakhsia kadhaa mashuhuri na muhimu nchini Afghanistan wakiwemo wanasiasa, wanaharakati, waandishi wa habari, madaktari na waendesha mashtaka wameuawa mchana kweupe mjini Kabul na katika miji mingine ya nchi hiyo.

Maafisa wa serikali wamekuwa wakilituhumu kundi la Taliban kuhusika na mauaji hayo, lakini kundi hilo linakanusha tuhuma hizo. Baadhi ya mauaji hayo yamekuwa yakihusishwa pia na kundi la kigaidi la ISIS.

Read Entire Article