PERMISSIONS

Italia yathibitisha habari ya kuuawa balozi wake Congo DRC katika shambulio la silaha

1 week ago 14

Wizara ya Mambo ya nchi za Nje ya Italia imethibitisha kuwa balozi wa nchi hiyo katikka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameuawa katika shambulizi la makundi ya waasi mashariki mwa Congo

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia imesema kuwa balozi Luca Attanasio ameuawa leo katika hujuma ya waasi dhidi ya msafara wa Umoja wa Mataifa karibu na eneo la Goma huko mashariki mwa nchi hiyo. Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa balozi Luca Attanasio na polisi mmoja wa Italia wameuawa katika hujuma iliyolenga msafara wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO) katika eneo la Kanyamahoro karibu na mji wa Goma.

Baada ya kupigwa risasi, balozi huyo wa Italia alikimbizwa hospitali na aliaga dunia kutokana na majeraha hayo.

Msemaji wa jeshi la Congo DR katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Meja Guillaume Djike amesema kuwa maafisa wengine wawili pia wameuawa katika hujuma hiyo lakini hakutaja utambulisho wao.

Askari wa Umoja wa Mataifa-Congo DR

Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Maeneo ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekuwa yakisumbuliwa na machafuko na uasi kwa zaidi ya miaka 20 sasa.  

Read Entire Article