PERMISSIONS

Israeli imetoa dozi 50,000 za chanjo ya COVID-19 zilizokwisha muda wake kwa wakazi wa Gaza

1 week ago 23

Wizara ya Afya ya Ghaza imesema kuwa utawala ghasibu wa Israel unapasa kubeba dhima kuhusu dozi elfu 50 za chanjo ya COVID-19 zilizokwisha muda wa matumizi zilizotolewa kwa eneo la Ukanda wa Ghaza linalosumbuliwa na mzingiro.

Wizara hiyo imesema kuwa, chanjo hizo zilihifadhiwa katika mazingira yasiyofaa na kwamba maafisa wa Israel walizuia shehena ya chanjo hizo kufika Ghaza kwa wakati. Taarifa ya Wizara ya Afya ya Ghaza imeeleza kuwa, chanjo hizo kutoka Russia aina ya Sputnik V ziliwasili Ghaza kupitia kivuko cha Karem Abu Salem, hata hivyo majaribio yaliyofanywa kuhusu usalama wa chanjo hizo yameonyesha kuwa zimekwisha muda wake. 

Awali vyombo vya habari vya Israel viliripoti kuwa, utawala huo ulikusudia kuipatia Mamlaka ya Ndani ya Palestina chanjo za corona ambazo muda wake wa matumizi ulikuwa ukikaribia kumalizika.

Takwimu zinaonyesha kuwa, Wapalestina 147,368 wameambukizwa corona huko Ghaza na wengine 1228 wamega dunia kwa ugonjwa huo. Hadi sasa Wapalestina wasiopungua 354,000 wamepata chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa COVID-19. Eneo la Ukanda wa Ghaza lina jamii ya watu wasiopungua milioni mbili.  

Wananchi wa Ghaza walio chini ya mzingiro 

Utawala haramu wa Israel umeshindwa kutimiza wajibu wake wa kuwapatia chanjo raia wa Kipalestina wanaoshi katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan na huko Ghaza inayokabiliwa na mzingiro. 

Read Entire Article