PERMISSIONS

Ijumaa tarehe 11 Juni 2021

3 months ago 4114

Leo ni Ijumaa tarehe 30 Mfunguo Mosi Shawwal 1442 Hijria sawa na tarhe 11 Juni 2021.

Katika siku kama ya leo miaka 449 iliyopita sawa na tarehe 11 Juni mwaka 1572, alizaliwa Benjamin Jonson mshairi na mwandishi wa filamu wa Uingereza. Jonson kwa muda mrefu alikuwa mcheza tamthilia na alikuwa rafiki wa Shakespare mwandishi maarufu wa Uingereza, ambapo urafiki wao ulikuwa na athari kubwa katika kukamilisha fasihi ya mshairi huyo. Baadhi ya athari zilizoachwa na Benjamin Jonson ni Mwanamke Aliyezimwa' pamoja na Historia ya Dunia. Malenga huyo Muingereza alifariki dunia mwaka 1637.

Benjamin Jonson

Siku kama ya leo miaka 166 iliyopita inayosadifiana na tarehe 11 Juni mwaka 1855, mwanga wa jua ulitambuliwa kwa kutumiwa njia za taaluma ya uchanganuzi na wigo wa rangi. Jaribio hilo lilifanywa kwa mara ya kwanza katika historia ya utafiti mpya wa fizikia na wanasayansi wawili wa Ujerumani walioitwa Kirchhoff na Bunsen. Si vibaya kuashiria hapa kwamba, mionzi ya jua katika hewa wakati wa mvua pamoja na kutokea upinde wa mvua wenye rangi mbalimbali, ni tukio la kuvutia ambalo linasababishwa na kuchanganuliwa nuru ya jua na matone ya maji mawinguni. Hata hivyo suala hilo mwanzoni lilifafanuliwa na wanasayansi wa Kiislamu kama vile Ibn Sina, Ibn Haitham na Qutbuddin Shirazi na baadaye kuthibitishwa na Kirchhoff na Bunsen.

Miaka 47 iliyopita katika siku kama ya leo sawa na tarehe 21 Khordad mwaka 1353 kwa mujibu wa kalenda ya Kiirani, alifariki dunia Daktari  Muhammad Khazaeli, mwasisi wa Tasisi ya Kuongoza na KuwasaidiaVipofu ya Iran.  Khazaeli alipokuwa mtoto alipoteza nguvu ya kuona kutokana na ugonjwa wa ndui, na alipata elimu katika shule maalumu ya vipofu. Dakta huyo kwa kutumia uwezo wake mkubwa wa kuhifadhi mambo, alipata mafanikio makubwa katika masomo yake na kufanikiwa kuhitimu shahada ya uzamilifu ya sheria katika Chuo Kikuu cha Tehran. Dakta Khazaeli alifahamu vyema lugha ya Kiarabu, Kifaransa na Kiingereza na aliandika na kutafsiri vitabu mbalimbali. Miongoni mwa masuala aliyojishughulisha nayo ni kupigania kupatiwa huduma muhimu vipofu katika uga wa kimataifa na alikuwa pia mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mashariki ya Kati katika Baraza la kitaifa la kuwahudumia vipofu na Jumuiya ya Kimataifa ya Vipofu.

Dakta Khaz'ali
Read Entire Article