PERMISSIONS

Hushpuppi – Mshawishi nyota wa Instagram aliyeiba mamilioni ya fedha

1 week ago 16

Dakika 9 zilizopita

Hushpuppi sitting on a red car - a photo posted on his Instagram account

Chanzo cha picha, hushpuppi

Ramon Abbas – anajulikana kwa mashabiki wake milioni 2.5 kwenye Instagram kwa jina la Hushpuppi – anachukuliwa na shirika la kijasusi la FBI kuwa tapeli mkubwa duniani akiwa anakabiliwa na kifungo cha miaka 20 nchini Marekani baada ya kukiri kufanya utapeli wa pesa .

BBC imetumia nakala mpya zilizopo mahakamani kugundua watu ambao walitapeliwa mamilioni ya fedha na tapeli huyo,

ambaye alianza kwa unyenyekevu kama “Yahoo Boy” ambaye anajaribu kuuza vitu mtandaoni nchini Nigeria mpaka kuja kuitwa “Billionaire Gucci Master” akiishi maisha ya kifahari Dubai kabla hajakamatwa mwaka jana.

Kijana huyo mwenye miaka 37-alianza kazi yake ya utapeli huko Oworonshoki, eneo la fukwe maskini lililopo kaskazini mashariki mwa mji wa Lagos nchini Nigeria.

Dereva wa eneo hilo kwa jina Seye aliiambia BBC kuwa anamkumbuka Abbas akiwa kijana mdogo akifanya kazi pamoja na mama yake katika soko la Olojojo. Baba yake alikuwa dereva wa magari ya kukodishwa(taxi).

Wakati anakuwa mkubwa , Seye anasema, Abbas alipenda magari ya kifahari : “Alikuwa mkarimu na alikuwa ananunulia bia kila mtu aliyekuwa karibu yake.

Lakini kila mmoja alifahamu kuwa chanzo cha utajiri wake wa kushangaza ulikuwa ni utapeli wa mtandaoni , alikuwa mtu wa “Yahoo”, Seye alisema.

Maelezo ya picha,

Makazi ya zamani ya Hushpuppi, alipokuwa na miaka 9 yapo katika mtaa wa Ogunyomi , eneo la Oworonshoki huko Lagos

“Yahoo Boys” ni matapeli wa mapenzi ambao walichukua jina lao katika barua pepe ya kwanza ya bure iliyopatikana Nigeria.

“Walikuja na wazo la kuiba utambulisho na kwa utambulisho huo , walienda kwenye programu za uongo za kutafuta wapenzi mtandaoni ,” alieleza Dkt Adedeji Oyenuga, mtaalamu wa masuala ya wizi mtandaoni kutoka chuo kikuu cha Lagos.

Wakati ambapo uhusiano ulipoanzishwa kwa kutumia utambulisho feki , wezi hao wa mtandao huanza kurubuni wapenzi wao wa mtandaoni kuwapa pesa .

Kama ilivyo kwa Yahoo Boys wengi , Abbas aliongeza mtandao wake wa uhalifu . Wengi huwa wanaenda Malaysia – na Abbas aliwafuata na kuishia Kuala Lumpur mnamo mwaka 2014, baadae akaenda kuishi Dubai mwaka 2017.

Wadukuzi wa Korea kaskazini

Huu ni wakati ambao alianza kutumia Instagram yake – na uhalifu wake ukapanda hadhi .

Mwezi Februari 2019,alifanya jaribio la kutapeli dola milioni 15 zilizoibwa na genge la wadukuzi wa Korea kaskazini kutoka benki ya Maltese ya Valley.

Abigail Mamo, mkuu wa chumba cha kusikilizia kesi ndogo na kati za biashara cha Maltese, anasema matapeli wakipanga kupumzika ufukweni hufanya hali kuwa mbaya.

Walijaza bidhaa kwenye troli na kuziacha kwa muuzaji endapo mfumo wa malipo uligoma.

“Tumepokea simu kutoka kwa wanachama wetu wakituambia wanalipa pesa kwa njia ya benki ya Valletta kwa wasambazaji wa nje ,” alisema bi. Mamo.

“Wasambazaji wa nje hawakupokea pesa … tunazungumzia kuhusu maelfu ya euros.”

Benki iliweza kufanikiwa kupata euro milioni 10.

“Damn,” Abbas alisema ujumbe mfupi kutoka kwa matapeli wenzake zilipatikana na FBI.

Majibu yalionesha walikuwa wamepanga njama nyingine : “Zoezi lingine litafanyika ndani ya wiki kadhaa; tutawafahamisha ni lini tukiwa tayari .Bahati mbaya yao wakakamatwa ingawa ,dili hilo lingewalipa vizuri sana.”

Kashfa dhidi yake

Mwezi Machi mwaka 2019, Abbas alipewa jukumu la kuanzisha akaunti nchini Mexico.

Ilikuwa ipokee £100m kutoka ligi ya Premia ya klabu ya soka, na £200m kutoka viwanda vidogo vya Uingereza.

Lakini haikuwa imeandikwa katika nyaraka zilizokuwa mahakamani .

Matapeli hao walitumia barua pepe ya biashara iliyojulikana kama Business Email Compromise (BEC).

Ilikuwa inatisha jinsi, BEC inavyofanya malipo feki kwa kutumia barua pepe ambayo inaonekana kama imetoka kwa muhusika mwenyewe kabisa.

Barua moja tu au namba inaweza kuleta utofauti.

Mtandao wa BEC ni mkuwa ukijihusisha na kujipatia kipato baada ya kutuma barua pepe zisizokuwa za kweli zikifanana na zile za kampuni ila tofauti inatokea kwenye namba moja tu.

Udanganyifu katika barua pepe inayotumwa inatuma ujumbe unaomtaarifu mtu kuwa kampuni husika imabadilisha banki ya kutuma fedha hizo kwahiyo inamhitaji atumie akaunti nyingine.

Karani wa Benki alaghaiwa na wezi wa mtandaoni baada ya kutumiwa ombi akifikiri limetoka kwa mtu anayemfahamu, alitumiwa na anasema unatumiwa kwenye kifaa chako cha mawasiliano na pale unapobonyeza mara moja tu , pesa yote inapotea.

Lakini ulaghai uliofanyika huku wahalifu hao wa kimtandao walijaribu kutumia jina la Waziri Mkuu haukuweza kufanyika baada ya Benki nchini Uingereza kugoma kufanya malipo. “Ndugu siwezi kutuma kutoka Uingereza kwenda Mexico,” Abbas alituma ujumbe huo.

Jon Shilland, Afisa kiitelejinsia masuala ya ulaghai wa kimtandao na Wakala wa Kitaifa nchini Uingereza, anasema kuwa sio rahisi kufuatilia majanga haya ya uhalifu wa kiulaghai yanayotokea kutokana na sheria za nchi nyingi.Wakili wa Dubai-Barney Almazar.

Anawakilisha karibu watu 25 – pamoja na raia wanane wa Uingereza – katika Falme za Kiarabu (UAE), ambao wote wanaamini kuwa ni wahanga wa utapeli wa BEC uliofanywa na Hushpuppi.

Chanzo cha picha, hushpuppi

Maelezo ya picha,

Uchunguzi unasema ni vigumu sana kupata mtandao wa matapeli kwa kuwa wapo dunia nzima

“Hatuwezi kusema kwa 100% kwamba Hushpuppi yuko nyuma yake,” Bwana Almazar anasema.

“Lakini ukiangalia akaunti za benki ambazo polisi wamefuatilia, zote ni za rekodi zilizopatikana na polisi katika uvamizi wao [nyumbani kwa Hushpuppi huko Dubai].”

Mtu mmoja wa Uingereza ambaye aliibiwa , alikataa kujulikana jina lake, anasema alipoteza Pauni 500,000, amelazimika kuondoka nchi za falme za kiarabu – na yeye mwenyewe anakabiliwa na kesi ya jinai huko Dubai kwa sababu ya deni ambalo amepata kama udanganyifu.

“Wateja wake wanaelewa kuwa alitapeliwa,” Bwana Almazar anaelezea.

“Lakini pia wanalazimika kujikwamua katika hasara walizopata, kwa hivyo kwa sasa hajui jinsi anavyoweza kurudi katika Falme za kiarabu. Maisha yake yote yalikuwa huko na familia yake bado iko Uarabuni. Anaogopa kwamba anaweza akakamatwa pindi tu anapoingia ofisi za uhamiaji. “

Bwana Almazar anasema ni aibu kuzuia wahanga wa utapeli wa Hushpuppi kuja kujieleza .

“Utapeli wake ulikuwa wa kiwango cha hali ya juu sana. Watu wenye elimu zao walitapeliwa. Wengine wanasita kukubali kile kilichotokea.”

Utapeli wa shule ya Qatar

Ulaghai mkubwa wa mwisho wa Abbas kabla ya kukamatwa kwake Dubai mnamo Juni 2020 ilikuwa wizi wa moja kwa moja, uliokopwa kutoka kwa utapeli wa mapenzi ya kijana wa Yahoo.

Alidhani utambulisho wa benki ya New York ili kumnasa tapeli wake, mfanyabiashara wa Qatar akitaka mkopo wa $ 15m kujenga shule mpya katika jimbo la Ghuba.

Kati ya Disemba 2019 na Februari 2020, Abbas na genge la watu wanaodaiwa kuwa watu wa kati nchini Kenya, Nigeria na Marekani walipanga njama ya kumtapeli zaidi ya dola milioni moja.

Utapeli mwingine ulijumuisha ununuzi wa saa yenye thamani ya dola 230,000 .

Lakini mvutano baina ya genge hilo ulianza.

Mjumbe mmoja alitishia kuripoti mtandao wote kwa kuwa akufurahishwa na fedha alizopata.

Abbas alijidhatiti kumnyamazisha awezavyo.

Alimtumia ujumbe afisa wa polisi wa Nigeria Abba Kyari – akisema: “Nataka umpe mateso makali sana katika maisha yake.

“Nataka kutumia ela kwa ajili ya huyu kijana kukaa jela kwa muda mrefu sana .”

Inadaiwa kuwa bwana Kyari alimkamata kijana huyo kwa madai ya uongo na akakaa gerezani nchini Nigeria kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Maelezo ya picha,

Abba Kyari,ambaye ni polisi , amesitishwa kazi na anatafutwa Marekani

Na sasa Bw Kyari pia anasakwa nchini Marekani kwa tuhuma za ulaghai, utakatishaji wa fedha na wizi wa kitambulisho.

Hapo awali alikanusha kuhusika katika utapeli wa Abbas – na hakujibu ombi la BBC la kutoa maoni.

Bado Instagram yake inavutia wafuasi

Ulaghai wa BEC ni suala kubwa ulimwenguni.

Kulingana na FBI, mnamo 2020 udanganyifu wa BEC ulisababisha upotezaji wa $ 1.8bn.

Nyaraka za mahakama zinadai uhalifu wa Abbas uligharimu wahanga karibu $ 24m kwa jumla. Lakini wengine wanaamini jumla halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.

Kwenye Instagram, “Bilionea Gucci Master” kwa “Msanifu Majengo” karibu miezi nane kabla ya kukamatwa kwake na baadaye kuhamishiwa Marekani kushtakiwa.

BBC

I have seen parents who have taken their children to learn how to become Yahoo boys”

Licha ya yeye kukiri kutapeli pesa mnamo Aprili , mitandao yake ya kijamii ya Hushpuppi bado inafanya kazi na inawavutia wafuasi wengi.

Tuliwasiliana na Instagram kuuliza ni kwanini akaunti yake ilikuwa bado wazi. Jukwaa la mitandao ya kijamii aliiambia BBC kwamba iliichunguza akaunti yake – lakini iliamua kutoifungia.

Siku chache tu baada ya kuuliza swali hilo kwa Snapchat, ambayo ilifuta akaunti ya Hushpuppi.

Dk Oyenuga anasema ushawishi wa Hushpuppi unadumu kwani bado anachukuliwa kama mfano wa kuigwa:

“Tuko katika taifa ambalo vijana wengi wanateseka na maisha. Wanaona kijana mwingine ambaye hapo awali alikuwa kama wao akawa tajiri mkubwa.

“Nimeona wazazi ambao wamechukua watoto wao kujifunza jinsi ya kuwa washirika wa ‘Yahoo boys’.”

Seye anasema kila mtu anajua Hushpuppi ametenda uhalifu, lakini inaeleweka: “Hakuna mtu anayeomba kuwa maskini. Kwa hivyo unapoona mtu tajiri, utamwomba Mungu akupe utajiri wa aina yake.

Read Entire Article