PERMISSIONS

Hali ya afya ya Mahmud Abbas

1 week ago 12

Rais wa Palestina Mahmud Abbas atangazwa kuwa katika hali nzuri kiafya baada ya kufanyiwa uchunguzi Ujerumani

Rais wa Palestina Mahmud Abbas, ambaye amepitia uchunguzi wa kimatibabu nchini Ujerumani,  amearifiwa kuwa yuko katika hali nzuri kiafya.

Kulingana na ripoti ya shirika rasmi la Palestina la WAFA, uchunguzi wa kimatibabu wa Rais Abbas uliokuwa ukifanyika nchini Ujerumani umekamilika.

Ilielezwa kuwa hakugundulika matatizo kwenye matokeo na Abbas alikuwa na afya njema. Maelezo zaidi yalibainisha kuwa Abbas atarejea Palestina hapo kesho.

Helikopta mbili za majeshi ya Jordan zilitua katika mji wa Ramallah ulioko Ukingo wa Magharibi mnamo Aprili 5 kumchukua Rais Abbas wa Palestina.

Ilielezwa kuwa Abbas, ambaye alipangwa kufanyiwa vipimo vya kawaida vya afya nje ya nchi, angepitia Jordan kwenda Ujerumani.

Abbas, mwenye umri wa miaka 85, alikuwa amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kwenye hospitali za Ukingo wa Magharibi ulioko chini ya uvamizi, na mji mkuu wa Amman nchini Jordan.

Read Entire Article