PERMISSIONS

Guterres asema ana wasiwasi kuhusu hali mbaya ya binadamu nchini Libya

2 months ago 3625

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa ana wasiwasi kuhusu hali mbaya ya masuala ya kibinadamu huko Libya.

Antonio Guterres amesisitiza kuwa nchi mbalimbali duniani zinapasa kuunga mkono mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Libya.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hayo baada ya duru za usalama za Libya kuripoti kuwa, Hussein al Ayeb Mkuu wa Idara ya Intelijinsia ya Libya amemkabidhi ripoti Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdul Hamid Mohammed Dbeibeh akitahadharisha kuhusu harakati za kundi la kigaidi la al Qaida zenye lengo la kutekeleza oparesheni ya kigaidi magharibi na kusini mwa Libya hususan katika miji ya Tripoli, al Zawiya na Sarman.  

Magaidi wa al Qaida huko Libya 

Ripoti ya Idara ya Intelijinsia ya Libya imeongeza kuwa, ukosefu wa amani unaoshuhudiwa katika miji ya magharibi mwa nchi unatumiwa na kundi la al Qaida kwa ajili ya kutekeleza mashambulizi katika maeneo hayo. 

Libya ilitumbukia katika hali ya mchafukoge na mgogoro wa kisiasa baada ya mapinduzi ya raia wa nchi hio mwaka 2011 yaliyomng'oa madarakani dikteta wa nchi hiyo, Kanali Muammar Gaddafi. Gaddafi aliondolewa madarakani kwa msaada wa majeshi ya nchi za Magharibi yakiongozwa na jumuiya ya NATO.

Read Entire Article