PERMISSIONS

Fahamu kwanini matukio ya ubakaji na ulawiti yameshamiri visiwani Zanzibar nchini Tanzania?

1 month ago 28

Dakika 9 zilizopita

Msichana akijifunika uso

Chanzo cha picha, AFP

Matukio ya udhalilishaji wa watoto kama ubakaji na ulawiti si jambo geni huko visiwani Zanzibar. Kwa mujibu wa UNICEF, asilimia 64 miongoni mwa kesi za udhalilishaji, ni udhalilishaji wa kingono kwa watoto visiwani humo.

Fatuma si jina lake halisi, alipata pigo baada ya mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 7 kulawitiwa na kijana mmoja ambaye alikua akifanya kazi saluni jirani na nyumbani kwao.

”Ndio nilikua nimemuanzisha shule, siku hiyo alitumwa na huyo kijana ambae alimfanyia kitendo cha udhalilishaji, ni jirani tu alimtuma kisha alimuahidi kitu Fulani akamlaghai na kumfanyia kitu cha kinyama” anasema Bi Fatma.

Bi Fatuma anasema kwa mujibu wa mwanae, siku ya tukio kijana huyo alimuita kisha kumtuma maji ya kunywa dukani, aporejea akamtuma tena kwa mara ya pili.

Baada ya kurudi, ndipo alipoanza kumfanyia kitendo hicho, wakati akiendelea na tukio hilo mmiliki wa saluni akaingia na kukuta hali hiyo.

Bi Fatuma anasema kuwa baada ya tukio hilo alimuwahisha mtoto wake hospitali kwa ajili ya vipimo, wataalamu wa afya walithibitisha kuwa ni kweli amefanyiwa udhalilishaji.

Baada ya hapo alikwenda polisi, mshukiwa wa kesi hiyo alishikiliwa kituo cha polisi kwa siku mbili kisha kuchiwa kwa dhamana.

Bi Fatma alifatilia kesi hiyo kwa muda mrefu, baada ya kuona hatakuna matumaini ya kwenda mahakamani anasema amemuachia Mungu

”Yupo tu mtaani anasubiri afanye tukio kama hili, lakini jambo moja la msingi mimi namuachia Mungu ndio muweza wa yote” anasema Bi Fatma.

Haya si matukio mapya masikioni mwa wakazi wa maeneo hayo.

Matukio ya udhalilishaji, kama kubaka na kulawiti, kuwakumba idadi kubwa ya watoto, wa kike kwa wa kiume.

Kwa mujibu wa utafiti wa Shirika linaloshughulikia watoto UNICEF, mtoto mmoja kati ya 10 wa kiume hukumbana na udhalilishaji wa kingono, na mmoja kati ya watoto wa kike 20 nae hukumbumbana na udhalilishaji wa kingono Zanzibar.

Mkuu wa wilaya ya mjini Unguja anasema kuwa ndani ya wiki moja wamepata matukio zaidi ya udhalilishaji wa watoto, na yanahusisha ndugu wa karibu kama baba kwa watoto wake.

Chanzo cha picha, Getty Images

”Tumeenda kumkamata mzazi mmoja amemlawiti mtoto wake, baada ya kwenda hospitali, akakutwa kuwa kitendo kile amekua akifanyiwa mara kwa mara, maana kila baada ya kufanyiwa kitendo kile anapitiwa na usingizi kabisa, tukio jingine baba amewalawiti na kuwabaka watoto wake wanne na yeye tumemkamata wiki hii” anasema Mkuu wa wilaya ya mjini Unguja Rashidi Msakara.

Katika kupambana na tatizo hilo, Rais wa Zanzibar Hussein mwinyi mapema mwezi uliopita alizitaka mamlaka za sheria nchini humo kuanzisha mahakama maalumu itakayohusiana na masuala ya udhalilishaji na pia kuwasilisha mabadiliko ya sheria katika baraza la wawakilishi la mwezi huu.

Mahakama hii itashughulikia kesi zote za uzalilishaji visiwani humo

Lakini kwanini kesi hizi zinaongezeka kila kukicha?

”Tatizo kubwa visiwani hapa ni suala la ‘muhali, Muhali maana yake ni kutofanya jambo ambalo linastahiki kulifanya lakini unaona tabu kulifanya, mfano aliyebaka ni baba kambaka mtoto, mama anakataa kumtoa baba kama mbakaji, mjomba anataka kesi iende lakini babu hataki, kwasababu aliyebaka ni mtoto wao, kwahiyo changamoto ndio hiyo” anasema mkuu wa wilaya ya mjini Unguja Rashidi Msakara.

Suala la muhali limekwamisha kesi nyingi za udhalilishaji kufikia mwisho na washukiwa kuhukumiwa vifungo vinanvyostahili.

Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi mapema mwezi uliopita alisema kuwa sheria za udhalilishaji zinapaswa kuchunguzwa na kurekebishwa ili kuondoa msongomano wa kesi za udhalilishaji kwenye vituo vya polisi na mahakama.

Maeneo gani vitendo vya udhalilishaji huwapata watoto?

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, maeneo ambayo watoto hupata udhalilishaji, ni njiani wakitoka nyumbani kwenda shule ama kurudi na madrasa.

Baadhi ya walimu wa madrasa wamepatwa ama kuhusishwa na kesi za udhalilishaji kwa watoto,

Kutokana visa kama hivyo, umoja wa walimu wa madrasa wameanzisha taasisi ya kutoa elimu kwa Umma ili kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa watoto.

”Taasisi hii tulianzisha, baada ya kuona kwanini walimu wa madrasa wanahusishwa na matukio haya na kweli baadhi wamekua wakifanya, kwa hiyo tukaona tuanzishe ili tutoe elimu kwa walimu, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa vitendo hivi,

havifai kabisa.” Anasema Khamisi Abdala Khamisi, afisa elimu wa jumuiya ya walimu wa madrasa Zanzibar.

Serikali na mashirika mbalimbali yameendelea kutoa elimu juu ya suala hili, lakini baadhi ya matukio ya udhalilishaji huhusisha imani za kishirikina, lakini pia mtendaji wa tukio akitokea kwenye familia, inakua ngumu kuchukuliwa hatua kwa sababu ya undugu.

Read Entire Article