PERMISSIONS

Corona ya Delta ndiyo iliyoenea zaidi hivi sasa nchini Nigeria

1 week ago 18

Waziri wa Afya wa Afya wa Nigeria, Osagie Ehanire amesema kuwa, aina ya Delta ya kirusi cha corona au UVIKO-19 ndicho kilichoenea zaidi katika nchi yenye watu wengi zaidi barani Afrika yaani Nigeria.

Tangu mwezi Juni mwaka huu, takwimu zinazotolewa na Kituo cha Nigeria cha Kudhibiti Magonjwa (NCDC) zinaonesha kuwa, sehemu kubwa ya wagonjwa wa corona ni wale wa kirusi cha Delta. Taarifa zinasema kuwa, hivi sasa serikali ya Nigeria inapigana na wimbi la tatu la maambukizi ya corona.

Waziri Ehanire amewaambia waandishi wa habari mjini Abuja kwamba, ushahidi uliopatikana hadi hivi sasa unaonesha kuwa kirusi cha corona aina ya Delta ndicho kilichoenea zaidi nchini Nigeria hivi sasa. Amesema, tunapaswa kuchukua hatua za kinga na kuongeza idadi ya watu wanaochukuliwa vipimo ili kukabiliana vilivyo na ugonjwa huo.

Zoezi la chanjo ya corona barani Afrika

Zaidi ya watu milioni 1.6 wameshapata chanjo kamili ya corona nchini Nigeria. Zoezi la kutoa chanjo hiyo lilianza miezi sita iliyopita katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Hayo yalisemwa Jumatatu wiki hii, na Faisal Shuaib, mkuu wa shirika la taifa la maendeleo ya kinga na afya la Nigeria, NPHCDA.

Takwimu za NCDC zinanesha kuwa Nigeria iligundua wagonjwa 387 wa corona siku ya Jumatatu sambamba na kuripoti vifo vya wagonjwa 21 wa UVIKO-19 siku hiyo. 

Pamoja na hayo, nchi za Afrika Kusini, Morocco, Tunisia na Ethiopia ndizo zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa na vifo vinavyotokana na UVIKO-19 barani Afrika.

Read Entire Article