PERMISSIONS

Corona: Tanzania na Zanzibar zavunja kimya chao

1 week ago 12

Baada ya kimya hicho hatimaye Serikali ya Zanzibar imetowa tamko la kuwataka wananchi kuchukuwa tahadhari kubwa dhidi ya maradhi mbalimbali ikiwemo tatizo la kupumuwa na virusi vya corona. Mwandishi wetu Salma Said ametuletea taarifa ifuatayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid Salum Mohammed ametaka kila mmoja kuchukua tahadhari kwa ajili ya kuyalinda maisha yake.

Katika siku za hivi karibuni Dk. Khalid amekiri kumejitokeza wananchi wengi ambao wanasumbuliwa na maradhi ya homa ya mapafu, homa kali na shida ya kupumua huku akiahidi kuwa serikali itafuatilia kwa karibu na kuchukua jitihada kubwa kupitia wataalamu wake ili kuidhibiti hali hiyo, na hapa anataja mambo muhimu za kuzingatia.

Rais Magufuli awataka wananchi kuacha kutumia barakoa zinazotoka nje ya nchi

Tansania Dar es Salaam | Gebet gegen Coronavirus

Rais wa Tanzania, John Magufuli hivi karibuni aliwataka wananchi kuacha kutumia barakoa zinazotoka nje ya nchi kwa sababu baadhi yake sio salama. Hata hivyo, Serikali ya Zanzibar imekwepa kueleza waziwazi suala hilo, lakini imesisitiza kutumia barakoa zinazotengenezwa nchini. Dk. Khalid tena.

Sambamba na hilo serikali ya Zanzibar imewashauri wananchi kuendelea kutumia dawa za kiasili kwa ajili ya kinga na tiba ya maradhi hayo kama anavyoeleza zaidi Dk. Khalid

Licha ya kutoa tahadhari kwa wananchi, serikali bado imesalia kimya kuhusu upimaji na utoaji wa takwimu za wagonjwa wa virusi vya corona baada kusitishwa zoezi hilo Aprili 2020. Tayari nchi za Uingereza na Oman zimewazuwia wasafiri kutoka Tanzania kuingia katika nchi hizo.

Read Entire Article