PERMISSIONS

Chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa Iran yaonyesha matumaini

1 week ago 14

Uchunguzi umebaini kuwa, chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa Iran ambayo inajulikana kama Razi Cov Pars haina madhara yoyote au hatari kwa mwanadamu.

 Dkt. Mohammad Hassan Fallah, Naibu Mkuu wa Utafiti na Teknolojia katika Taasisi ya Chanjo ya Razi ambayo imeunda chanjo hiyo, amesema chanjo hiyo imeonyesha matumaini makubwa. Amesema hadi kufikia tarehe 5 Aprili watu 120 walikuwa wamepokea dozi ya kwanza na watu wengine 42 wamepokea dozi ya pili ya chanjo ya Razi Cov Pars katika awamu inayondelea ya majaribio. Amesema matokeo ya uchunguzi wa chanjo hiyo ya Razi Cov Pars yatafikishwa katika Shirika la Dawa na Chakula katika kipindi cha siku chache zijazo na baada ya kupokea vibali vinavyohitajika, awamu ya pili ya majaribio itaanza.

Chanjo ya Fakhra

Amesema hadi sasa waliopokea chanjo hiyo hawajapata madhara yoyote na wako katika hali nzuri kiafya.  Chanjo ya Razi Cov Pars inatajwa kuwa moja ya chanjo ambazo hazina hatari duniani na sababu ya hilo ni kuwa katika kipindi cha majaribio waliodungwa chanjo hiyo hawajakumbwa na matatizo yoyote.

Iran iko mstari ya mbele kuunda chanjo za COVID-19 ambapo mbali na  chanjo ya Razi Cov Pars, chanjo zingine ambazo zimepiga hatua nzuri katika majaribio ni pamoja na COV Iran Barakat,  Fakhra na chanjo ya pamoja ya Taasisi ya Chanjo ya Finlay ya Cuba na Taasisi ya Chanjo ya Pasteur ya Iran.

Read Entire Article