PERMISSIONS

Brazil yaweka rekodi mpya ya vifo vya Corona, zaidi ya 4,000 waaga dunia

1 week ago 14

Kwa mara ya kwanza tangu janga la Corona liikabili dunia mapema mwaka jana, zaidi ya watu 4,000 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Covid-19 nchini Brazil katika kipindi cha siku moja.

Wizara ya Afya ya Brazil imetangaza jana Jumanne kuwa, watu 4,195 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa Corona katika kipindi cha saa 24 nchini humo.

Kwa mujibu wa takimu za Chuo Kikuu cha John's Hopkins, watu zaidi ya 366,000 wameaga dunia kwa maradhi hayo hatarishi ya kuambukiza kufikia sasa katika nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Baada ya kupita karibu mwaka mzima tangu Shirika la Afya Duniani WHO iutangaze ugonjwa wa Covid-19 kuwa ni janga la dunia, bado Brazil ina idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ugonjwa huo, suala ambalo limeitia wasiwasi mkubwa jamii ya kimataifa.

Brazil inavyohangaishwa na janga la Corona

Wataalamu wa afya nchini humo wanakosoa sera na misimamo ya Rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro juu ya janga la Corona, licha ya kiongozi huyo binafsi kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19 Julai mwaka jana.

Mtawala huyo mwenye utata wa Brazil amekuwa akipuuzilia mbali janga la Corona akiutaja ugonjwa huo kuwa mafua tu yasiyokuwa na athari kubwa, huku akipinga kuchukuliwa hatua na kuwekwa sheria kali za kudhibiti msambao wa maradhi hayo nchini humo.

Read Entire Article