PERMISSIONS

Bleir: Uislamu hauna uhusiano na misimamo mikali na chuki

1 week ago 23

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza amesema kuwa dini ya Uislamu haina mfungamano na ugaidi, chuki na misimamo ya kuchupa mipaka na amewahimzia Waislamu kukabiliana na chuki na misimamo mikali.

Tony Blair ameashiria mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 huko Marekani ambayo yalifanyika katika kipindi cha utawala wake huko Uingereza na kusema: "Naamini kuwa makundi yenye chuki na misimamo mikali ndiyo yaliyotekeleza mashambulizi ya Septemba 11." Bleir amesisitiza kuwa dini ya Uislamu haihusiki na chuki na misimamo mikali. 

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza ameongeza kuwa, kwa sasa kumeanzishwa mapambano halisi katika Ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya ugaidi. 

Tarehe 11 Septemba mwaka 2001 ndege nne za abiria zilitumiwa na kundi la watu 19, wengi wao wakiwa raia wa Saudi Arabia, kushambulia miji ya New York na Washington huko Marekani. Watu karibu elfu tatu walipoteza maisha katika mashambulizi hayo. 

Baada ya mashambulizi hayo, rais wa zamani wa Marekani, Goerge W. Bush alikhitari siasa na sera za kuhujumu nchi mbalimbali kwa kisingizio cha mapambano ya kimataifa dhidi ya ugaidi.

Maelfu ya raia wa Afghanistan wameuawea katika mashambulizi ya Marekani

Zaidi ya watu milioni moja wameuawa katika nchi za Iraq, Afghanistan, Syria, Libya na Yemen katika vita hivyo vya Marekani eti 'dhidi ya ugaidi'. 

Read Entire Article