PERMISSIONS

Balozi wa Italia DRC auawa kwenye shambulizi

1 week ago 17

Balozi wa Italia Luca Attanasio na mwanajeshi mmoja wauawa kwenye shambulizi dhidi ya msafara wa wajumbe wa UN

Balozi wa Italia Luca Attanasio na mwanajeshi mmoja wa Italia wameripotiwa kuuawa kwenye shambulizi lililoendeshwa dhidi ya msafara wa Umoja wa Mataifa (UN) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia, iliandikwa,

"Tunathibitisha kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanajeshi wa Italia na Luca Attanasio ambaye ni Balozi wa Italia katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo."

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa shambulizi hilo lilitokea wakati Balozi Attanasio na mwanajeshi mmoja kutoka kikosi cha jeshi la Italia walikuwa wakisafiri kwa gari kwenye msafara wa MONUSCO, ambao ni wajumbe wa UN wa kudumisha amani na utulivu nchini DRC.

Katika taarifa za vyombo vya habari vya Italia, iliarifiwa kuwa baada ya shambulizi la msafara wa UN, washambuliaji walijaribu kuwateka nyara wajumbe.

Read Entire Article