PERMISSIONS

Amnesty yazikosoa nchi tajiri kwa kujilimbikizia chanjo ya corona

1 week ago 15

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekosoa sera za ukiritimba za nchi tajiri duniani na jinsi zinavyojilimbikizia chanjo ya kukabiliana na virusi vya corona.

Ripoti ya kila mwaka ya Amanesty International iliyotolwa leo Jumatano imesema kuwa, nchi tajiri zimeshindwa na kufeli katika mtihani wa awali kabisa wa mshikamano ya kimataifa kwa siasa zao za ukiritimba na kujilimbikizia chanjo ya corona, huku zikiitumu China na nchi nyingine kuwa zinatumia vibaya maambukizi ya corona kwa ajili ya kudhoofisha haki za binadamu.  

Katibu Mkuu wa Amnesty International, Agnès Callamard ametoa wito wa kuharakishwa ugavi wa chanjo ya corona kote duniani na kusema kuwa, mlipuko wa maambukizi ya corona umedhihirisha udhaifu wa dunia na kushindwa kuonyesha ushirikiano athirifu na wa kiadilifu. 

Callamard ameongeza kuwa, nchi tajiri zimehodhi ugavi wa chanjo ya virusi vya corona duniani na kuziacha nchi maskini zikiendelea kuzongwa na kusumbuliwa na athari mbaya zaidi za mgogoro wa kiafya na haki za binadamu. 

Awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema kuwa maambukizi ya virusi vya corona ni changamoto kubwa ya karne ya sasa. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekosoa namna chanjo ya corona inavyozalishwa na kugawiwa baina ya nchi mbalimbali duniani na kusema: Asilimia 75 ya chanjo ya corona imegawiwa katika nchi 10 tu duniani huku zaidi ya nchi 100 zikisalia bila ya chanjo.  

Read Entire Article