PERMISSIONS

Amnesty: Jeshi la Ethiopia liliua mamia ya raia Ethiopia Novemba

1 month ago 24

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amesty International limesema mauaji ya kiholela ya mamia ya raia yaliyofanywa na jeshi la Eritrea katika mji wa kale wa Ethiopia wa Axum Novemba mwaka jana ni ukiukaji wa wazi wa haki za binadamu na ukanyagaji wa sheria za kimataifa za kumlinda mwanadamu.

Ripoti iliyotolewa leo Ijumaa na Amnesty International imesema kuwa, mnamo Novemba 28 na 29 mwaka uliopita 2020, wanajeshi wa Eritrea kwa makusudi na mpangilio maalumu waliwaua mamia ya raia katika mji wa Axum, yapata kilomita 187 kaskazini mwa Makelle, makao makuu ya eneo la Tigray.

Mauaji hayo ya halaiki yalifayika wakati wa mapigano baina ya pande mbili za jeshi la serikali ya Ethiopia na vikosi vya Harakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Tigray TPLF.

Kwa mujibu wa shirika la Msamaha Duniani, wanajeshi wa Eritrea walitekeleza unyama huo kwa lengo la kuwafanya wakazi wa mji huo wawapigie magoti na wajisalimishe kwao.

Waasi wa TPLF eneo la Tigray

Mashuhuda na manusura 41 wa mauaji hayo ya halaiki wameiambia Amnesty International kuwa, mbali na mauaji, wanajeshi hao wa Eritrea pia waliiba mali na milki za wakazi hao. Amnesty International imesema mauaji na wizi huo vinaweza kuwa jinai za kivita.

Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, maelfu ya watu wameuawa na wengine karibu milioni moja wamelazimika kukimbia makazi yao kaskazini mwa Ethiopia kutokana na mapigano hayo ya eneo la Tigray. 

Read Entire Article