PERMISSIONS

Afghanistan:Je ni rais gani wa Marekani aliyehusika na kufeli kwa taifa hilo Afghanistan?

1 week ago 21

14 Septemba 2021, 14:56 EAT

mm

Chanzo cha picha, Reuters

Miongo miwili iliyopita jeshi la Marekani lilifanikiwa kuliondoa kundi la Taliban katika utawala nchini Afghanistan.

Lakini kwasasa majeshi hayo hayo ya Marekani yameondoka na Taliban imefanikiwa kurudisha serikali yake.

Bado kuna wasiwasi mkubwa kwa nchi ya Afghanstan kuw ngome ya vikundi vya kigaidi.

Ndani ya miongo miwili, marais wanne wa Marekani waliweza kufanya maamuzi sahihi zilizohusu taifa la Afganistan.

Swali ni Je, Rais yupi wa Marekani ndiye muhusika mkuu wa kutofaulu katika operesheni za kijeshi nchini Afghanstan?

George Bush

Chanzo cha picha, Reuters

Tarehe 11 Septemba 2001, magaidi wenye msimamo mkali waliteka nyara ndege nne.

Ndege hizi zilitumika kwenye shambulizi katika Kituo cha biashara cha dunia cha New York, Pentagon na Pennsylvania.

Aliyewahi kuwa mshauri wa serikali ya Marekani na pia Balozi wa Marekani nchini Afghanstan Michael McKinley anasema kuwa “Wakati mashambulizi yalivyotokea nilikuwa Mantralaya, tulitazama nje ya dirisha. Moshi mkubwa ulionekana tuliamua kutoka lakini hatukuwa tunajua chochote kilichokuwa kinaendelea.”

Wanamgambo walifanya shambulizi siku ya 9/11 lilikuwa ni shambulio kubwa kuwahi kutokea katika historia ya Marekani.

Waliohusika zaidi ni kundi la kigaidi lenye mismamo mikali la Al Qaeda wakishirikiana na baadhi ya raia wa Afghanstan.

Shambulio hilo liliuwa watu 2,977 huku 6,000 wakijeruhiwa vibaya.

Kulenga al Qaeda Miaka michache kabla ya shambulizi hilo Marekani ilianza kutilia shaka ukaribu wa kundi la al Qaeda na Taliban, kundi lilikuja kuchukua hatamu miaka mitano awali.

Chanzo cha picha, Getty Images

Shambulizi hili limeonekana kubadili siasa za Marekani.

Michael McKinley anasema, “Ilitarajiwa kwamba Marekani itapata njia ya kujilinda. Ilijibu kwa nguvu mashambulio ya 9/11.”

“Tukio hili liliilazimisha Marekani kufikiria jinsi ya kufanya kazi na washirika wake katika ardhi ya kigeni na jinsi ya kukabiliana na matishio yaliokuwa yakitokea. Mabadiliko ambayo yamefanyika katika sera ya mambo ya nje ya Marekani katika kipindi cha miaka 20 iliyopita yamehusishwa na uamuzi wa Bush.

Ilikuwa ni miezi michache tu tangu George Bush awe Rais wa nchi hiyo. Kwa hivyo mkakati wao ulikuwa nini kujibu mashambulio hayo?

Michael McKinley anasema, “Iliamuliwa kutoa uamuzi kwa serikali ya Taliban. Iliulizwa kuwapa watu waliohusika na shambulio hilo kwa Marekani na iiruhusu ithibitishe kuwa hakuna misingi ya itikadi kali nchini.”

Kulikuwa na uungwaji mkono kutoka kwa raia baada ya Marekani kuanza kampeni yake nchini Afghanistan, vyama vya upinzani vilishiriki kikamilifu na kupanga mikakati madhubuti kwa nchi yao.

Disemba mwaka 2001 serikali ya Kitaliban iliangushwa.

Kundi la kigaidi la Al Qaeda liliamua kukimbilia nchini Pakistan, mpango huu wa Marekani ulionekana kuwa wenye manufaa zaidi.

Chanzo cha picha, CPL JOHN SCOTT RAFOSS/MOD CROWN COPYRIGHT/PA WIRE

Vita ya Iraq

Ilikuwa rahisi kuishinda Taliban baada ya jeshi  kuingilia kati, lakini ilikuwa ngumuzaidi kwa Afghanstan kuunda serikali.

Kabla ya utawala wa Bush kushughulikia changamoto hii, Machi 2003, Jambo jipya liliibuka kwenye serikali yake.  Bush aliamua kuanzisha vita dhidi ya Iraq. 

Utawala wa Bush haukugundua ni jinsi gani inaweza kuwa ngumu kujenga nchi. Kama matokeo, kasi ya maendeleo nchini Afghanistan ilianza kuyumba na ufisadi ulianza kuongezeka.

Michael McKinley anasema, “Baadhi ya viongozi wa Taliban walitaka kujisalimisha, wengine walitaka kuwa sehemu ya serikali mpya. Lakini uwezekano wa kutumia fursa hii ilipuuzwa kabisa.”

Kwa mara nyingine kundi la Taliban likaanza kushupaza kichwa kwa Marekani. Katika muhula wa pili wa Rais Bush,aliamuru majeshi yake kupambana na kundi hilo.

Kwa majibu wa kitabu cha Ahmed Rashid cha Taliban: The Power of Militant Islam in Afghanistan and Beyond, kilichochapishwa mwaka 2004, Taliban walifanya mashambulio sita. Mwaka 2005 idadi ya mashambulio iliongezeka hadi 21 na  2006 iliongezeka mara nyingi kufikia idadi  ya 141. 

Chanzo cha picha, CORPORAL ADRIAN HARLEN/MOD/PA WIRE

Marekani iliamua kuongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Afghanistan na kuimarisha jeshi la Afghanistan, lakini bado kulikuwa na changamoto.

Marekani iliweza kushinda, lakini haikuwa na mpango wa wazi kuondoa majeshi yake.

Barack Obama

Chanzo cha picha, Getty Images

McKinley anasema, “Kulikuwa na mkakati wa swali. Jambo hili liliweza kubadilisha mtazamo wa kisiasa. Watu wa nje hawakuielewa vizuri. Mtu hapaswi tu kuangalia kile wageni walifanya.

Inapaswa pia kuonekana kile viongozi walifanya huko. ” Barack Obama Profesa Paul D. Miller aliwahi kuwa mkurugenzi wa wafanyakazi wa Baraza la Usalama la Kitaifa dhidi ya Afghanistan na Pakistan wakati wa utawala wa Rais Bush. 

Alikuwa katika nafasi hii kwa mwaka mmoja wakati wa Rais Obama. vile vile amefanya kazi na Jeshi la Marekani pamoja na shirika la ujasusi la CIA.

Miller anasema kuwa katika kampeni ya uchaguzi Obama aliunga mkono hatua za kijeshi nchini Afghanistan.

Anasema, “Katika hotuba yake mwaka 2008, Obama alizungumzia sera za kigeni bila kuisahau Afghanistan na akasema kwamba hii ni vita muhimu ambayo inapaswa kushinda kwa njia zote.”

Lakini baada ya kuwa rais  Januari 2009, Obama aliendeleza zaidi kile alichoanzisha Rais Bush.

 Idadi ya wanajeshi wa kigeni nchini Afghanistan ilikuwa imefikia elfu 37.

Muda mfupi baadae  Obama alibadilisha mkakati wa vita dhidi ya ugaidi nchini Afghanistan. Profesa Miller anasema, “Obama alisema kwamba atatuma wanajeshi zaidi kushughulikia visa vinavyoongezeka vya ghasia. Aliiita mkakati wa kupambana na uasi (COIN) na kampeni ya kujenga imani ya umma kwa serikali ya Afghanistan.”

“Nadhani ulikuwa mkakati sahihi. Kupitia hii serikali ya kudumu inaweza kuundwa huko. Lakini utawala wake ulikabiliwa na changamoto mbalimbali.”

Chanzo cha picha, Reuters

Kuna kipindi ilionekana kulikuwa na ripoti za udanganyifu mkubwa katika uchaguzi wa Afghanistan ambapo kulizuka ghasia. 

Jenerali Stanley McChrystal, kamanda wa jeshi la Marekani aliyekuwa nchini humo, alimsihi rais atume wanajeshi zaidi na akasema kwamba wasipofanya hivyo “juhudi za kumaliza ugaidi zinaweza kufaulu.”

Mwaka 2009, Obama aliidhinisha kutuma wanajeshi 17,000 nchini Afghanistan mwezi Februari na wengine 30,000 Disemba. 

Jeshi la Majini la Marekani ilitoa taarifa za kumuua Osama bin Laden huko Pakistan.

Na kampeni kuu ya Marekani dhidi ya Taliban na al-Qaeda ilikuwa imekwisha.

 Obama alitangaza kuondoa majeshi yake. Biden alikuwa makamu wa Rais kipindi hiki. 

 Profesa Miller anasema kuwa shida ilianzia hapo kwani anaamini kuwa teyari Taliban walikuwa wameishiwa nguvu.

“Wakati Marekani ilipotangaza kuondoa majeshi yake, Taliban walipata matumaini ya kurudisha dola lake. Tangazo la Rais Obama lilibadilisha taswira nzima ya vita nchini humo.

“Kile ambacho jeshi lilikuwa limefanikiwa kufikia sasa ilikuwa kama kudhoofisha. Nadhani hali ya sasa ilianza wakati wa utawala wa Obama.” Lakini kwa wakati huu ukweli ulikuwa umejitokeza wazi kuwa shida iliyotokea Afghanistan haikuweza kutatuliwa. “Hakujua kuwa huu ungekuwa mpango wa muda mrefu na wenye gharama kubwa,” anasema Profesa Miller.

Donald Trump

Chanzo cha picha, Reuters

Pojesha DeGenera ametumika kama mshauri mwandamizi wa kijiografia wa serikali ya Marekani na jeshi. Anasema, “Trump hakuwa na wasiwasi juu ya kile kinachotokea nyuma. Yeye mwenyewe alichukua maamuzi juu ya jinsi ya kushughulika na nchi zingine.

 Hakuwa na nia ya kuendeleza vita huko Afghanistan. Alianza mipango ya kurudisha majeshi yake.

” Msaada mkubwa ambao utawala wa Bush ulikuwa umepokea juu ya suala la Afghanistan sasa ulikuwa umepungua. Raia wa kawaida hawakutaka tena Marekani kuwalinda. 

Rais Trump alifanya kile ambacho hakuna rais kabla yake alikuwa amefanya.

Pojesha anasema, “Alichukua uamuzi wa upande mmoja na akaanza mazungumzo na Taliban bila kushauriana na washirika wake. Alichagua pia tarehe ya kuhamishwa kwa wanajeshi. Washirika walikubaliana nayo.” 

“Mkataba ulifikiwa na Taliban na kuwekewa sharti kwamba hawatashambulia wanajeshi wa kigeni. Lakini kulikuwa na kasoro nyingi katika makubaliano haya. Moja, mashambulio kwa wanajeshi wa kigeni na raia hayakukoma, na pili, serikali ya Afghanistan ilikuwa hakuhusika katika mazungumzo.

Chanzo cha picha, Reuters

Wape ujasiri Taliban Trump alisema anaamini Taliban, wamechoka na mizozo ya kila wakati,alikuwa na imani kuwa watatii masharti ya makubaliano hayo. 

Pojesha anasema, “Nadhani Trump mwenyewe hakuweza kuelewa hali hiyo. Pia alishindwa kuchagua wataalam ambao walielewa hali hiyo na chanzo chake.” 

“Idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan haikuwa siri tena. Taliban ilikuwa ikijiandaa kuchukua madaraka na Pakistan pia ilikuwa ikijiandaa kwa sababu ya mabadilikoyanayotokea upande huo. Trump alifanya makubaliano na viongozi wa Taliban lakini walipuuza kuhusu Pakistan. 

Makubaliano kati ya Marekani na Taliban yalitangazwa mwanzoni mwa mwezi Februari 2020.

Makubaliano haya pia yalitumika kwa vikosi vya NATO vikifundisha vikosi vya usalama vya Afghanistan, ambao walitakiwa kuondoka Afghanistan na vikosi vya Marekani ifikapo 1 Mei 2021.

Kulingana na makubaliano hayo,Marekani iliwaachilia huru wafungwa wapatao 5,000, ambao wengi wao walijiunga na Taliban. Taliban nao waliwaachilia wafungwa 1,000.

Kipindi Trumpa akiwa rais, kulikuwa na askari 8,500 wa Marekani  huko Afghanistan. Baadae idadi yao iliongezeka hadi 13,000. Mwisho wa kipindi cha Trump, takwimu hii iliongezeka hadi 2500.

 Pojesha DeGenera anasema kuwa uamuzi wa kuwaleta wanajeshi nyumbani haukuwa mbaya, lakini ungeweza kufanyika kwa njia bora. Anasema, “Uamuzi wake wa kuondoka Afghanistan ulikuwa sahihi. Shida ilikuwa kutekeleza uamuzi waliokubaliana nao, na kisha ilibidi ampe jukumu hilo kwa serikali ijayo

Profesa Christine Fair ni profesa wa masomo ya usalama katika chuo kikuu cha Edmund A. Walsh , shule ya masomo ya kigeni .

Alienda Afghanistan mwaka 2007 kama afisa wa kisiasa wa misheni ya Umoja wa mataifa.

Anaamini kuwa bila kumtaja Biden ambaye alikuwa makamu wa rais katika utawala wa Obama, jukumu lake haliwezi kujadiliwa kwa wakati huu.

Christine anasema maoni ya Biden juu ya Taliban na Afghanistan hayana tofauti na ya Obama. Anaamini kuwa kulenga Taliban haina maana.

Alisema , “Biden anaamini kuwa Taliban si tishio kwa Marekani kama al-Qaeda. Hataki kuweka uadui na Taliban .Anataka kumaliza operesheni ya kuwatokomeza wanachama wa al-Qaeda.

“Lakini kwa sasa hali ni kwamba bila uwepo wa askari wa Marekani nchini humo, mpango huo hauwezi kukamilika. Pia itakuwa vigumu kupata jasusi kutoka hapo. Wale ambao wanasema kuwa Biden anafuata tu makubaliano yaliyofanywa na Trump, Amekosea. Hicho ndio alitaka kukifanya kama Makamu wa Rais miaka iliyopita. “

Chanzo cha picha, Reuters

‘Biden angeweza kubadili maamuzi ya Trump’

Christine amekiri kuwa makubaliano ya Trump yalikuwa na mapungufu mengi lakini haiwezekani kusema kuwa Biden hausiki na kile kinachoendelea Afghanistan.

Biden angeweza kubadili maamuzi ya Trump, lakini hakutaka kufanya hivyo.

Alisema, “Watalibani wamerudia kuvunja ahadi yao . Biden angeweza kuachana na makubaliano hayo , Biden hakuwahi mkosoa Trump kwa kupeleka idadi kubwa ya wanajeshi . Ingawa ndio hivyo Trump ameyafanya aliyoyafanya.”

Biden aliongeza tarehe ya kuondoa wanajeshi wake nchini Afghanistan kuanzia Mei 1 mpaka Septemba 11. Baadae akasema mwisho Agosti 31.

Siku chache kabla, Biden alisema Taliban hawawezi kuidhibiti Afghanistan hivi karibuni. Lakini siku chache tu Taliban iliweza kudhibiti taifa lote la Afghanistan.

Shinikizo kutoka kwenye uchaguzi

Christine anasema kuwa suala la Marekani kukaa zaidi nchini Afghanistan ilikuwa kinyume na madhumuni ya utawala wa Biden na hakutaka kushiriki katika vita visivyo na mwisho.

Anasema, “Kuna mazungumzo katika Chama cha Democrats kwamba kabla ya katikati ya muhula wake , Biden anapaswa kufanya kazi ya maendeleo na kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.”

“Tofauti ya idadi kati ya Republican na Democrats katika Seneti na Baraza la Wawakilishi ni ndogo. Katika hali kama hiyo, Biden lazima azingatie uchaguzi. Wataalam wengine wanaamini kuwa hii ni sababu kubwa nyuma ya machafuko yaliyoonekana nchini Afghanistan.

Sasa ukirudi kwa swali la… Ni nani anayehusika na kushindwa kwa mipango ya Marekani huko Afghanistan?

Vita vya Iraq vilikuwa kipaumbele kwa utawala wa Bush badala ya ujenzi wa Afghanistan, uamuzi wa Obama wa kuondoa wanajeshi uliwapa Taliban ujasiri, Taliban walipata zaidi ya ilivyotarajiwa katika makubaliano ya Trump, na kisha kile kilichotokea katika siku za hivi karibuni, Biden alishindwa kuona yeye.

Marais hao wanne walitegemea sana uongozi wa kisiasa nchini Afghanistan na waliidharau Taliban.

Katika hali kama hiyo, tunaweza kusema kwamba wote wanne wanawajibika kwa kiwango fulani kwa hali ambayo imetokea Afghanistan katika kipindi cha hivi karibuni.

Nini kilitokea wakati wa operesheni ya jeshi la Marekani huko Afghanistan?

Septemba 11, 2001 – Ndege nne ziligongana na majengo katika miji tofauti ya Marekani. Hizi ni pamoja na Minara Miwili ya New York na Pentagon huko Washington.

Oktoba 2001 – Rais wa zamani wa Marekani George Bush alizindua Operesheni ya Uhuru wa Kudumu. Alitangaza mashambulizi dhidi ya a al-Qaeda katika vikosi vya Marekani na Uingereza.

Novemba 2001 – Vikosi vya kigeni vilianza kuwasili nchini Afghanistan. Awamu ya kwanza, askari 1,300 wa Marekani walifika Afghanstan.

Disemba 2001 – Wanajeshi wa Marekani walizunguka milima ya Tora-Bora kutafuta mahali aliko mkuu wa al-Qaeda ,Osama bin Laden.

Kulingana na ripoti zingine, Bin Laden alikimbia na kujificha katika eneo la Pakistan mnamo Disemba 16.

Lakini, kulingana na ripoti zingine, Bin Laden alitoroka mnamo Disemba 11. Kufikia sasa idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ilikuwa 2,500.

Maelezo ya picha,

Hamid Karzai

Disemba 2001 – Wataliban wanaingia madarakani na mchakato wa kuunda serikali ya mpito chini ya Hamid Karzai huko Afghanistan.

Machi 2002 – Kwa lengo la kukomesha kabisa visa vya kukithiri, jeshi la Marekani linaanza kuchukua hatua mpaka kuungana na vikosi vya usalama vya Afghanistan.

Disemba 2002 – Idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan iliongezeka hadi 9,700.

Mei 2003 – Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Donald Rumsfeld alisema kwamba operesheni kubwa nchini Afghanistan imeisha na kwamba nchi hiyo sasa itaelekea kwenye utulivu. Kwa upande mwingine, Marekani ilitangaza vita dhidi ya Iraq.

Januari 2004 – Afghanistan ilipata katiba yake mpya.

Aprili 2004 – Marekani ilituma wanajeshi zaidi kulinda miradi ya maendeleo iliyokuwa inaendelea nchini Afghanistan na kuongeza vituo katika mpaka wa Afghanistan na Pakistan. Mwisho wa mwaka, idadi ya wanajeshi wa Marekani iliongezeka hadi 20,300.

Oktoba 2004 – Hamid Karzai akawa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia katika uchaguzi. Wakati huohuo, ujumbe wa video wa Osama bin Laden uliibuka.

Disemba 2006 – Vita na Iraq vikawa kipaumbele cha Wamarekani. Katika hali kama hiyo, idadi ya wanajeshi nchini Afghanistan ilipunguzwa hadi 20,000.

Januari 2009 – Barack Obama alichukua nafasi ya urais. Kwa wakati huu idadi ya wanajeshi wa kigeni nchini Afghanistan ilikuwa imefikia 37,000. Obama aliidhinisha kutuma wanajeshi 17,000 nchini Afghanistan mnamo Februari mwaka huu, halafu wengine 30,000 mnamo Disemba.

Disemba 2009 – Utafutaji wa Osama bin Laden uliongezeka. Kufikia sasa idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ilikuwa ilifikia 67,000.

Agosti 2010 – Idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan ilipita alama moja ya laki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eneo ambalo Osama aliuliwa

Mei 2011 – Marekani ilipokea taarifa kutoka kwa vyanzo vya ujasusi kwamba Osama bin Laden yuko Pakistan.

Baada ya hayo, kama sehemu ya operesheni ya ujasusi, mnamo Mei 1, Bin Laden aliuawa na Mihuri ya Jeshi la Majini la Marekani huko Abbottabad, Pakistan.

Juni 2011 – Obama anasema “Ujumbe wa Marekani huko Afghanistan umetimia”. Alisema kuwa mwishoni mwaka 2011, jeshi la Marekani lingejiondoa hapa.

Septemba 2012 hadi Disemba 2014 – Mchakato wa kuanza kuwaondoa askari wa Marekani kutoka Afghanistan ulianza.

Wakati huo kulikuwa na askari 77,000 mnamo Septemba 2012, kulikuwa na 46,000 mnamo Disemba 2013, 34,000 mnamo Machi 2014 na 16,100 tu mnamo Disemba 2014.

Disemba 2014 – Obama alisema jeshi litawawezesha wanajeshi wa Afghanistan kwa kuwafundisha.

Oktoba 2015 – Barack Obama alisema hali hiyo sio sawa kabisa kwa kuondoka kabisa kutoka Afghanistan.

Alisema kulikuwa na wanajeshi 9,800 kwa operesheni ya kupambana na uasi ifikapo 2016, na baada ya hapo idadi hiyo ikapunguzwa hadi 5,500 kufikia Disemba 2016.

Julai 2016 – Obama alisema hali ya nchini Afghanistan bado ina wasiwasi. Alisema kuwa badala ya kuongeza idadi ya wanajeshi kufikia 5,500, wanajeshi 8,400 wa watakuwepo hapo.

Agosti 2017 – Trump alisema kuona hali ya nchini Afghanistan, askari zaidi watapelekwa huko. Aliamua kuongeza idadi ya wanajeshi hadi 14,000.

Februari 2020 – Makubaliano muhimu yalifikiwa kati ya Marekani na Taliban, ambayo chini yake ilikubaliwa kupunguza uwepo wa wanajeshi Wamarekani nchini Afghanistan.

Novemba 2020 – Serikali ya Marekani ilisema kwamba kufikia katikati ya Januari mwaka ujao, idadi ya wanajeshi nchini Afghanistan itaongezwa hadi 2,500 na kisha kufikia Mei 1, 2021, jeshi lao litajiondoa kabisa kutoka Afghanistan.

Aprili 14, 2021 – Rais Joe Biden alisema kuwa kulingana na makubaliano kati yao na Taliban, vikosi vyao vitaondoka Afghanistan sio ifikapo Mei 1, 2021, lakini ifikapo Septemba 11, 2021.

Julai 8, 2021 – Rais Joe Biden alisema kuwa kufikia Agosti 31, 2021, jeshi la Marekani litaondolewa kabisa nchini Afghanistan.

Agosti 15, 2021 – Baada ya kukamata majimbo kadhaa ya Afghanistan, Taliban iliteka mji mkuu Kabul. Rais wa nchi hiyo Ashraf Ghani aliondoka nchini na kwenda Falme za Kiarabu.

Agosti 31, 2021 – Vikosi vya Marekani viondoka kabisa kutoka Afghanistan. Jenerali Kenneth McKinsey wa Jeshi la Marekani alitangaza hii huko Pentagon

Read Entire Article