PERMISSIONS

Abdulhamid al-Dabaiba: Libya kudumisha uhusiano imara na Uturuki

1 month ago 18

Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Libya amesema kuwa serikali mpya ya mpito ya nchi hiyo itatoa umuhimu makhsusi kwa uhusiano kati ya nchi hiyo na Uturuki.

Abdulhamid al-Dabaiba amesema kuwa, uhusiano kati ya Libya na Uturuki utakuwa imara na kupewa kipekee. Amesema Uturuki ni mshirika wa kiuchumi wa Libya na kwamba Tripoli inaunga mkono suala hilo. Waziri Mkuu wa Libya ameseyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari huko Tripoli. 

Abdulhamid al-Dadaiba aidha amesisitiza udharura wa Libya kufungamana na makubaliano ya masuala ya baharini kati yake na Uturuki yaliyofikiwa mwezi Novemba 2019. Katika mkutano huo na vyombo vya habari, Waziri Mkuu wa Libya aidha amesema tayari amewasilisha orodha ya majina mapya ya mawaziri wa serikali mpya katika bunge la Tobrok ili kupigiwa kura ya kuwa na imani nao. 

Amesema, serikali mpya ya Libya inawakilisha watu wa rangi, makabila na matabaka yote na kwamba serikali hiyo mpya itafanya kazi ya kutatua matatizo makubwa yanayowasumbua wananchi wa Libya.   

Itakumbukwa kuwa, Baraza la Mazungumzo ya Libya lililofanyika huko Geneva chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa lilimchagua Abdulhamid al-Dabaiba kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo, Mohamed Yunus al-Menfi kuwa Mkuu wa Baraza la Urais, na Abdullah Hussein Al Lafi na Musa Al Koni walichaguliwa kama wajumbe wawili wa baraza hilo.  

Katika hotuba yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa, Waziri Mkuu wa Libya, Abdulhamid al-Dabaiba alisema kuwa, baraza lake la mawaziri litaheshimu uwazi na uwajibikaji na litafanya juhudi kubwa za kutatua mtatizo ya nchi ikiwa ni pamoja na tatizo la umeme na kutayarisha chanjo ya corona.

Abdulhamid al Dadaiba Waziri Mkuu wa Libya  
Read Entire Article